1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mazungumzo ya mkataba wa kushughulikia majanga yaanza tena

5 Novemba 2024

Mataifa yalikutana tena Jumatatu kwa lengo la kukamilisha makubaliano ya kihistoria ya kimataifa juu ya kushughulikia magonjwa ya milipuko ya siku zijazo.

Mkuu wa Shirika la Afya Duniani -WHO- Tedros Adhanom Ghebreyesus wakati wa mkutano wa mawaziri wa afya wa G20 .
Mkuu wa Shirika la Afya Duniani -WHO- Tedros Adhanom GhebreyesusPicha: Ajit Solanki/AP/dpa/picture alliance

Wakati wa ufunguzi wa mazungumzo hayo, katibu mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, aliwaambia waakilishi wa mataifa hayo kwamba wanakabiliwa na jukumu la kukamilisha majukumu yao kwa wakati ufaao na pia kufikia makubaliano madhubuti.

Ghebreyesus aonya janga litakalofuata halitasubiri mazungumzo

Ghebreyesus, aliongeza kuwa muda umeyoyoma na kwamba virusi vya Uviko19 bado vinasambaa, ugonjwa wa mpoxni dharura ya kimataifa ya afya na kwamba pia kuna mripuko wa ugonjwa wa marburg na H5N1, akiongeza kuwa janga litakalofuata halitasubiri.

Ugavi wa chanjo kujadiliwa baadaye

Baada ya zaidi ya miaka miwili ya mazungumzo, matumaini ni makubwa ya kukamilisha makubaliano hayo ifikapo Novemba 15, ingawa suala kuu la jinsi ya kugawanyachanjo linatarajiwa kufanyiwa kazi baadaye.