1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
KandandaUlaya

Real timu ya kwanza kuifunga Barcelona

26 Oktoba 2026

Real Madrid imekuwa timu ya kwanza kuifunga Barcelona katika Ligi Kuu ya Uhispania La Liga msimu huu.

LaLiga 2026/27 | Real Madrid vs. Sevilla | Kylian Mbappé asherehekea kufunga bao la tatu
Kylian Mbappe wa Real Madrid akisherehekea kufunga baoPicha: Violeta Santos Moura/REUTERS

Hii ni baada ya kuilaza timu hiyo 2-1 huko Camp Nou Jumapili huku Kylian Mbappe akifunga mabao mawili.

Mabao hayo mawili yalimpelekea Mbappe kufikia jumla ya mabao 11 katika mechi 10 za La Liga alizocheza msimu huu na ulikuwa ushindi wa kwnaza wa Jose mourinho katika mechi za El Clasico tangu aliposhiriki kama kocha mara ya mwisho miaka 13 iliyopita alipokuwa kocha wa Real Madrid.

Nafasi nzuri za kufunga kwa timu zote

"Ilikuwa mechi ngumu sana dhidi ya mpinzani mkali," Mourinho aliwaambia waandishi wa habari. "Kwetu sisi ni ushindi uliopatikana kutokana na mchezo mzuri zaidi."

Kocha wa Real Madrid Jose MourinhoPicha: picture alliance / ASSOCIATED PRESS

Timu zote mbili zilibuni nafasi nzuri za kufunga ila mashambulizi ya Madrid ndiyo yaliyozaa matunda.

Mbappe aliwafungia Madrid bao la kwnaza kisha Raphinhaakawasawazishia Barca kunako kipindi cha pili na mechi ilipokuwa inaelekea mwisho, Mbappe akaongeza la pili la Madrid baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Jude Bellingham na Eduardo Camavinga.

Kushindwa huku kwa Barca kunakuja baada ya kulazwa 4-2 na PSG katikati ya wiki huko mjini Paris katika Ligi ya Vilabu Bingwa na kocha Hansi Flick amesema hii ndiyo iliyokuwa sababu ya wachezaji wake kuonekana kuishiwa na nguvu katika mechi hiyo.

Msururu wa mechi ulichangia uchovu

"Ni kushindwa mara mbili na hatujafurahia," Flick aliwaambia waandishi wa habari. "Tumeshushwa mabega, tulikuwa tumechoka."

Kocha wa Barcelona Hansi FlickPicha: Matthieu Mirville/ZUMA Press/picture alliance

Licha ya kushindwa, Barcelona wanasalia kileleni mwa La Liga wakiwa na pointi 27 kutokana na mechi 10, pointi moja mbele ya Atletico Madrid walio katika nafasi ya pili. Madrid wanaoishikilia nafasi ya tatu wana pointi 24.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW