1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoPoland

Mbappe aanza vyema Madrid, wakichukua ubingwa wa Super Cup

15 Agosti 2024

Mshambuliaji Kylian Mbappe ameanza vyema kuitumikia klabu yake mpya ya Real Madrid kwa kufunga bao moja kati ya mawili yaliyoiwezesha klabu hiyo kuchukua ubingwa wa UEFA Super Cup.

UEFA SUPER CUP 2024 Real Madrid Atalanta Bergamo Mbappe
Mshambuliaji wa Real Madrid Kylian Mbappe baada ya kuifungia bao katika mechi yake ya kwanza na kikosi hicho na kuisaidia kuchukua ubingwa wa UEFA Super CupPicha: Czarek Sokolowski/AP Photo/picture alliance

Real Madrid iliishinda Atalanta kwa mabao 2-0 katika mechi iliyochezwa jana Jumatano huko mjini Warsaw, Poland.

Mbappe aliifungia Madrid bao la pili katika dakika ya 68, baada ya kupewa pasi na Jude Bellingham. Bao la kwanza lilifungwa na Fede Valverde.

Mbappe amesema baada ya mchezo huo kwamba, huu ni wakati aliousubiri kwa hamu na ni zawadi kubwa kucheza akiwa na jezi ya Madrid, ambao pia ni mabingwa wa UEFA Champions.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW