Mbappe asema anaanza upya baada ya kipindi kigumu
23 Desemba 2024Mbappe aliongeza msururu wake wa mabao kwa kupachika wavuni bao maridadi kabisa katika ushindi wa 4-2 wa Real Madrid dhidi ya Sevilla katika ligi kuu ya uhispania jana. Bao hilo lilikuwa lake la sita karika mechi zake nane za mwisho akiwa kwenye uzi wa Madrid.
Alipata wakati mgumu tangu alipojiunga na klabu yake hiyo mpya, lakini sasa anaonekana kuwa Mbappe aliyefufuka. Kocha wake Carlo Ancelotti anasema sasa nyakati ngumu zimekwisha. "Ni mwepesi wa kujikosoa ili kurekebisha mambo na hilo ni muhimu. Amejitokeza akionyesha ujuzi wake. Nilisema jana kwamba muda wake wa kuzoea maisha umekwisha na alionyesha leo kwamba wakati mwingine, niko sahihi."
Madrid wanamliza mwaka pointi moja nyuma ya vinara Atletico Madrid. Atleti walitoka nyuma na kuwafunga Barcelona 2 – 1. Barca sasa wako nafasi ya tatu pointi mbili nyuma ya Madrid, wakiwa wamecheza mechi moja ya ziada.