1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mbappe akiri timu yake haikucheza kwa viwango

15 Julai 2026

Ufaransa yaambulia patupu kwenye mchuano wa nusu fainali dhidi ya Uhispania. Lakini je Uhispania inatosha kutwaa kombe la dunia

Mbappe akijizatiti kutafuta bao kwenye nusu fainali ya kombe la dunia bila mafanikio dhidi ya Uhispania
Mbappe akijizatiti kutafuta bao kwenye nusu fainali ya kombe la dunia bila mafanikio dhidi ya UhispaniaPicha: Christopher Neundorf/EPA/IMAGO

Nahodha wa Ufaransa, Kylian Mbappe, amesema timu yake ilionesha mchezo wa  kiwango cha chini na kufanya makosa mengi yaliyoipa Uhispania nafasi ya kuitoa kwa ushindi wa mabao 2-0 katika nusu fainali ya Kombe la Dunia iliyochezwa Arlington, Texas.

Mbappe amesema Uhispania ilitamba na kudhibiti mchezo kwa kuachia wachezaji wengi zaidi katikati ya uwanja, hali iliyowapa Rodri na Fabian Ruiz fursa nzuri ya kuongoza mchezo, na kukiri kwamba Ufaransa ilikosa mawasiliano katika kuikaba timu ya Uhispania.Wachezaji 10 wa kufuatilia Kombe la Dunia 2026

Ufaransa iliingia nusu fainali ikiwa imeshinda mechi zake zote sita za awali na kufunga mabao 16, lakini ilishindwa kutengeneza nafasi nyingi dhidi ya Uhispania.

Mikel Oyarzabal aliifungia Uhispania bao la kwanza kwa mkwaju wa penalti kabla ya Pedro Porro kufunga la pili na kuipeleka timu hiyo fainali.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW