1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mbio za kumtafuta kiongozi mpya wa CDU zashika kasi

Angela Mdungu
26 Februari 2020

Kati ya yaliyoandikwa na wahariri wa magazeti ya hapa Ujerumani leo (26.02.2020) ni kuhusu mbio za kugombea uongozi wa chama cha CDU, na hukumu ya mmoja wa watayarishaji maarufu wa filamu wa Marekani Harvey Weinstein

Bundestag Debatte Iran-Abkommen Norbert Röttgen
Mmoja wa wagombea wa uenyekiti wa chama cha CDU Norbet RöttgenPicha: picture-alliance/dpa/B. Pedersen

Gazeti la Stuttgatter Nachrichten linasema huenda mgombea asiyepewa nafasi kubwa ya kurithi kiti cha AKK ndani ya CDU, Norbert Röttgen akaibuka mshindi mwisho wa siku. Hivi sasa kinyang'anyiro hicho kinaonekana kuwa zaidi kati ya kiongozi wa zamani wa CDU Friedrich Merz na waziri kiongozi wa Nordrhein Westphalia Armin Laschet.

Mhariri wa gzeti la Frankfurter Rundschau ameandika juu ya hukumu ya aliyewahi kuwa mtayarishaji mkubwa wa filamu nchini Marekani Harvey Weinstein. Gazeti hilo linaandika, kitendo cha jopo la majaji wa mahakama ya juu mjini New York kumkuta na hatia ya makosa ya ubakaji na udhalilishaji wa wanawake ni mafanikio makubwa. Si tu kwa wanawake ambao Weinstein aliwadhalilisha bali pia ni kwa wale waliopata moyo wa kupaza sauti zao kupitia kampeni ya #Metoo.

Kuhusu ulinzi zaidi katika Misikiti

Berliner Morgenpost limeangazia kuimarishwa kwa ulinzi  katika misikiti hapa Ujerumani. Gazeti hilo limeandika, baada ya shambulio la mjini Hanau jamii haina budi kuzoea kwamba sasa maafisa wa polisi wanasimama mbele ya misikiti mjini Berlin kwa sababu jamii ina tatizo la ubaguzi.

Mamlaka za usalama zinapaswa kuchukua hatua zenye matokeo yanayoonekana kwa kuanza kupambana na shughuli zinazofanywa na watu wanaofuuata itikadi za mrengo wa kulia. Hawana budi kuwafuatilia na kuwadaka watu wanaofanya mambo hayo  wakiwa nyuma ya kompyuta zao.

Ostthüringer Zeitung limeandika kuhusu virusi vya Corona likiangazia namna ya kujikinga na virusi hivyo limeanza kwa kuandika ni muhimu kwa watu kuwa na tabia za mtu anapopiga chafya ama kukohoa hana budi kuweka umbali kidogo na watu wa pembeni yake. Usikohoe ama kupigachafya moja kwa moja kwenye viganja vyako bali kwa kutumia kitambaa unachoweza kukitupa katika chombo cha taka chenye mfuniko. Na  kama unadhani kufanya hivi ni rahisi jiulize ni kwa nini virusi vinavyosababisha mafua kila mwaka vimekuwa havizuiliki.

Mwandishi: Angela Mdungu / inlandspresse

Mhariri: Sekione Kitojo

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW