Freeman Mbowe, aliyekuwa mwenyekiti wa CHADEMA kwa miongo miwili amekiri kushindwa katika uchaguzi wa uenyekiti wa chama hicho na kumpongeza Tundu Lissu kupitia mtandao wa kijamii wa X. Lissu alitangazwa mshindi leo baada ya zoezi la upigaji kura lililofanyika usiku kucha katika mkutano wa wajumbe wa taifa wa chama hicho jijini Dar es Salaam, Tanzania.