MBS kufanya ziara Marekani Novemba 18
4 Novemba 2025
Matangazo
Ziara hiyo inakuja wakati ambapo Trump anaishinikiza Saudi Arabia kujiunga na orodha ya nchi ambazo zilitia saini mikataba wa Abraham, inayolenga kusawazisha mahusiano baina ya Israel na mataifa kadhaa ya Kiarabu.
Mwaka 2020 Trump alikubaliana na Umoja wa Falme za Kiarabu, Bahrain, Sudan na Morocco kusawazisha mahusiano yao na Israel.
Lakini Saudi Arabia qimesita kujiunga na orodha hiyo kutokana na kukosekana kwa hatua zitakazolifanya Palestina kuwa taifa huru.
Ila katika mahojiano Jumapili iliyopita, Trump alisema ana matumaini kuwa saudi Arabia itajiunga na mikataba hiyo.