1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mchakato wa kuandikisha wapiga-kura Zimbabwe ni changamoto

Admin.WagnerD8 Julai 2013

Wakati wananchi wa Zimbabwe wakijiandaa kwa uchaguzi mkuu Julai 31 mwaka huu zaidi ya raia 50 wa nchi hiyo wameshindwa kusajiliwa katika daftari la wapigakura kwa madai kuwa sio raia na wazee kutakiwa kuleta uthibitisho

Kundikisha Zimbabwe wapiga kura Zimbabwe
Kundikisha Zimbabwe wapiga kura ZimbabwePicha: Reuters

Kiongozi wa wafanyakazi wa Waziri mkuu Morgan Tsvangirai, Lan Makone ameliambia shirika la habari la IPS kuwa watu wengi Nchini Zimbabwe wamezuiliwa kujisajili katika daftari la kupigia kura.

Mtandao wa Zimbabwe unaoshugukilia uchaguzi, ambao ni muungano wa mashirika yasiokuwa ya serikali kwa ajili ya kufuatiliaa uchaguzi umesema uasili wa uandikishaji katika daftari la kupigia kura, mazingira yaliofunmgamna na zoezi hilo, vitisho dhidi ya wanaharakati wa kiraia ni jaraibio la Chama cha Rais Robert Mugabe cha ZANU-PF kuchochea machafuko katika uchaguzi ili  kutetea uhalali wake wa kisiasa.

Rais Mugabe amekuwa mdarakani kwa muda wa miaka 33 katika utawala ambao umekithiri kwa rushwa, machafuko na mbinyo wa kisiasa

ZANU-PF yadaiwa kupanga ugumu huo

Taasisi ya Youth Agenda Trust mtandao wa shirika la vijana nchini Zimbabwe umeongeza kuwa  mchakato huo wa usajili wa watu ulipangwa makusudi ili kuwanyima raia wa Zimbabwe haki yao ya msingi ya kupiga kura.

Rais wa Zimbabwe Robert MugabePicha: Reuters

Akiongea na shirika la habari la IPS mkurugenzi wa shirika hilo Fortune Nyamanda amesema hatua ya kuwanyima watu kuandikisha majina yao kwa madai ni wageni, ni kuwanyima haki yao ya kikatiba raia wa Zimbabwe ya kupiga kura kama ilivyoelezwa katika kifungu cha katiba mpya ya Zimbabwe.

Hayo yanafanyika wakati marekebisho ya 12 ya kifungu cha sheria ya mwaka 2011, kuhusu watu wenye urai wa sehemu mbili,Katiba hiyo mpya ambayo imezinduliwa mwzi Mei baada ya mzunguko wa kwanza wa usajili wa wapiga-kura, inatambua raia waliozaliwa nje ya Zibabwe  na wazazi wa Zimbabwez wanatambuliwa kama raia wa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa takuimu za ofisi ya mjini Harare kwa ajili ya Mashirika ya kimataifa kuhusu uhamiaji, kati ya raia 500,000 na milioni nne wa Zimbabwe wanaishi nje ya nchi. Wengi wao wamekimbia hali ya uchumi kati ya mwaka 2003 na 2009. Zimbabwe ni nchi hyenye kiwango kibaya kabisa cha mfumko wa bei  ulimwengu.

Kama ilivyo kwa wapiga kura wengine wenye kutaka kupiga kura,  Emilia Magirazi mwenye umri wa miaka 27 katika baridi ya asubuhi alilazimka kusubiri ili kujiandikisha kama mpiga kura katika foleni iliokuwa inaenda taratibu katika shule ya msingi ''Kuwadzana 8'' iliopo mji mkuu wa nchi hiyo Harare.

Mzunguko wa pili wa uandikishaji wapiga kura nchini Zimbabwe umenza Juni 19 mwaka huu na unatarajiwa kuisha leo hii Jumanne Julai 9 wakati uchaguzi mkuu ukitarajiwa kufanyika Julai 31-2013 ambapo mzunguko wa mwanzo ulifanyika siku 20 ndani ya mwezi wa Aprili na Mei.

Lakini watu kama Magirazi wanajikuta katika wakati mgumu kuweka majina yao chini katika mchakato huo wa uchaguzi wa Zimbabwe hii ni kwa sababu yeye ni raia wa kigeni alizaliwa Zambia lakini wazazi wake ni wazimbabwe.

Magirazi anasema kuwa alifika katika kituo cha kujiandikisha mapema Asubuhi lakini lakini hadi kufikia wakati wa chakula mchana alifanikiwa kupata huduma ambapo makarani walimuambia yeye si raia na hivyo hata weza kuandikisha jina lake na kupelekwa kituo cha polisi ili kutafuta kibali na maelezo iwapo anahusika katikamakosa ya jinai.

Mwandishi: Hashim Gulana/IPS

Mhariri: Mohammed Khelef