1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mchezaji wa kutoka China awa shujaa katika Derby Catalonia

Sekione Kitojo
6 Januari 2020

Mchezaji kutoka China awa shujaa katika Derby ya barcelona na maashindano ya Super Cup ya Uhispania yatafanyika nchini Saudi Arabia yakishirikisha timu nne, Barcelona, Real Madrid, Valencia na Atletico Madrid

Spanien La Liga Santander - Espanyol v FC Barcelona | Wu Lei
Picha: Reuters/A. Gea

Bao  la  dakika  za  mwisho  la  kusawazisha  kwa Espanyol  dhidi  ya  Barcelona  liliashiria  ukurasa  mpya  katika kandanda  la  Uchina, vyombo  vya  habari  vya  nchi  hiyo  vilisema jana, baada  ya  tukio  hilo  la  kishujaa  kusambaa  mitandaoni nchini  humo.

Mchezaji  huyo wa  timu  ya  taifa  ya  China  Wu Lei  aliingia dimbani  akitokea  benchi  na  kupachika  bao  katika  dakika  ya  88 ambalo lilileta sare ya  mabao 2-2 kwa  timu  hiyo  iliyochini  ya msimamo wa  ligi  ya  La Liga katika  pambano  la  watani  wa  jadi, derby, siku  ya  Jumamosi.

Mashabiki wa Barcelona wakiwa uwanjani Camp NouPicha: picture-alliance/dpa/AP Photo/E. Morenatti

Ushindi  mfululizo  wa  michezo  mitano  wa   Real Sociedad  ulifikia mwisho jana  katika  ligi  ya  Uhispania  baada  ya  kupata  kipigo cha  mabao 2-1 dhidi  ya  Villarreal  na  kupoteza  mwelekeo  katika mbio za  kupata  nafasi  katika  champions League.

Barcelona  na  Real Madrid  zinafungana  juu  ya  msimamo wa  ligi zikiwa  na  pointi 40  kila  moja, ambapo klabu  hiyo  kutoka  jimbo  la Catalonia  iko  mbele  kwa  tofauti  ya  magoli.

Wakati huo huo  mashindano  ya  Super Cup  nchini  Uhispania yaliyopewa msukumo  mpya  yanaaza  siku  ya  Jumatano nchini Saudi Arabia, hatua  ambayo  itaongeza  kipato  kwa  shirikisho  la kandanda  nchini  humo  lakini  imeyakasirisha  makundi  ya  haki za binadamu  na  mashabiki nchini  humo. Real madrid  na  Valencia zinakutana katika  nusu  fainali  ya  kwanza  mjini  Jeddah siku  ya Jumatano  kabla  ya  barcelona  kupambana  na  Atletico Madrid masaa  24  baadaye siku  ya  Alhamis, fainali  itafanyika  siku  ya Jumapili.

Wachezaji wa FC Barcelona wakishangilia bao lililowekwa wavuni na Antoine Griezmann(katikati)Picha: picture-alliance/dpa/AP/J. Monfort

Super Cup  ilikuwa  ni  mchezo wenye mikondo miwili kati ya mabingwa  wa  ligi  na  kombe  la  taifa  Copa del Rey lakini  mkuu wa  shirikisho la  kandanda  Luis Rubiales  aliendesha mabadiliko makubwa  Novemba  mwaka  jana , akipata  makubaliano ya  miaka miwili  kuchezesha  mashindano  hayo nchini  saudi Arabia.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW