1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mchungaji aliyepotosha kuhusu corona Uganda ashikiliwa

30 Machi 2020

Mahakama nchini Uganda imempeleka rumande mchungaji aliyetoa matamshi ya kupotosha kwamba hakuna virusi vya corona Afrika, matamshi yanayodhoofisha juhudi za kupambana na kusambaa kwa virusi hivyo.

Flagge Uganda
Picha: picture-alliance/blickwinkel/McPHOTO/K. Steinkamp

Mchungaji huyo ni miongoni mwa viongozi wa kidini zaidi ya 20 waliokamatwa mwishoni mwa wiki kwa kukiuka maagizo yanayolenga kukabiliana na janga la COVID-19. 

Ijapokuwa viongozi wa kidini nchini Ugandawaliazimia kuisadia serikali katika kuhakikisha kuwa maagizo yanayolenga kuepusha kuenea kwa ugonjwa wa COVID-19 yanatakelezwa, kuna baadhi kama mchungaji Augustine Yiga ambao wanapotosha umma kwa kukanusha madhara ya ugonjwa huo.

25.03.2020 Matangazo ya Mchana

This browser does not support the audio element.

Mchungaji huyo ameshtumiwa vikali kwa kuhatarisha maisha ya watu na kukwaza juhudi za kuhamasisha kila mtu ashiriki katika kukabiliana na janga hilo. Viongozi wengine 25 walikamatwa mwishoni mwa wiki kwa kukiuka maagizo ya kuepusha mikusanyiko. Polisi ambayo mwanzoni ilitumia nguvu za kupindukia kukabiliana na wale waliokiuka maagizo inafanya juhudi kuhamasisha watu. Kulingana na msemaji wa polisi eneo la Kampala Patrick Onyango kila mtu ambaye anapotosha umma kuhusu suala ya mrikupo wa COVID-19 atachukuliwa hatua. 

Polisi nchini Uganda wanwashikilia viongozi hao wa kidini kwa kukiuka masharti ya vita dhidi ya coronaPicha: DW/E. Lubega

Vyombo vya usalama vimeunda jopokazi la pamoja kushirikiana na wafanyakazi wa afya katika kuwafuatilia washukiwa wa ugonjwa huo waliotoroka kutoka karantini. 

Miongoni mwa waliokwepa karantini ya siku kumi nan ne ni wanasiasa wakiwemo mawaziri 6 na jamaa zao waliotokea ng'ambo. Kundi hilo limelezewa kuwa tishio kubwa kwa umma huku rais Museveni akiwazuia mawaziri hao kutoshiriki vikao vy baraza la mawaziri. Raia wa kawaida Ibrahim Kakeeto amesema hivi kuhusu vitendo vya watu hao mashuhuri.

Katika habari zingine, hii leo rais Yoweri Museveni wa Uganda na viongozi wenzake wa shirikisho la maendeleo kanda ya pembe ya Afrika IGAD wamefanya mkutano kwa njia ya video kujadili mikakati ya pamoja ya kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19.Hadi wakati wa kuandaa taarifa hii, Uganda imeripoti kuwa visa 33 vya ugonjwa.

Lubega Emmanuel DW Kampala

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW