1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mecca, Saudi Arabia. Hija yaanza.

28 Desemba 2006

Kiasi Waislamu milioni mbili wamekusanyika katika eneo la Mina, karibu na mji wa Mecca, nchini Saudi Arabia wakianza hija ya kila mwaka.

Maafisa wameongeza ulinzi kutokana na hofu ya mashambulizi ya kigaidi pamoja na mtafaruku.

Mwaka jana tukio hilo la Hija limeshuhudia watu 360 wakiuwawa kutokana na mkanyagano.

Kila Muislamu ambaye anajiweza kiafya na kifedha analazimika kwenda Hija mjini Mecca, mahali alipozaliwa Mtume Mohammad, SAW, takriban mara moja katika uhai wake.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW