1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoSaudi Arabia

Mechi za Kombe la Dunia ngazi ya Vilabu kuchezwa Jeddah

26 Juni 2023

Shirikisho la kandanda duniani FIFA limesema kuwa mechi za Kombe la Dunia mwaka 2023 ngazi ya vilabu zitachezwa mjini Jeddah, Saudi Arabia.

FIFA Klub-Weltmeisterschaft | Sieger Real Madrid
Real Madrid wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kuchukua ubingwa wa Kombe la Dunia ngazi ya vilabu kufuatia ushindi wao dhidi ya Al Hilal.Picha: 900/Cordon Press/picture alliance

Hii ni baada ya wajumbe wa FIFA kufanya ziara katika mji huo ili kukagua maandalizi yanayoendelea kuelekea mechi hizo.

Mashindano hayo yatafanyika Disemba 12 hadi 22, na hii itakuwa ni kwa mara ya kwanza kufanyika nchini humo.

"Tunaamini kwamba kuandaa hafla za michezo ya kimataifa kama Kombe la Dunia la Vilabu kutatoa fursa kwa mchezo huo kukuwa zaidi na kuibua hamasa mpya miongoni mwa mashabiki wa kandanda, pamoja na kuonyesha ukarimu, utamaduni wa Saudi Arabia duniani,” ameeleza Rais wa shirikisho la kandanda la Saudi Arabia Yasser Al Misehal.

Saudi Arabia, kama ilivyokuwa kwa waandaji wa Kombe la Dunia la FIFA 2022 Qatar, imekosolewa vikali kutokana na visa vya ukiukaji wa haki za binadamu, hivi karibuni imekuwa ikijiweka katika nafasi ya kuandaa mashindano ya kimataifa ya michezo.

Soma pia:Infantino: Mizozo ikome wakati wa kombe la dunia 

Nchi hiyo imehusishwa na kutuma ombi la kuandaa Kombe la Dunia la FIFA la mwaka 2030.

Kombe la Dunia ngazi ya vilabu ni mashindano ya kimataifa ya kandanda inayokutanisha mabingwa wa mashirikisho sita ya bara, pamoja na mabingwa wa ligi kuu ya taifa linaloandaa mashindano hayo.

Toleo la mwaka 2023 litakuwa la mwisho lenye kujumuisha timu saba kabla ya mashindano hayo kupanuliwa hadi timu 32 mnamo mwaka 2025 na yatakuwa yanayofanyika kila baada ya miaka minne.

 

 

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi