1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kombe la Dunia: Senegal na Ubelgiji zapata ushindi mnono

27 Juni 2026

Michuano ya Kombe la Dunia imeendelea kutimua vumbi katika viwanja mbalimbali huko Marekani, Canada na Mexico.

Toronto I Mechi kati ya Senegal na Iraq
Mechi kati ya Senegal na Iraq katika michuano ya Kombe la Dunia huko Toronto, CanadaPicha: Nathan Denette/The Canadian Press/AP Photo/picture alliance

Siku ya Ijumaa, Iran iliilazimisha Misri sare ya 1-1, huku Ubelgiji ikipata ushindi wake wa kwanza kwa kuicharaza New Zealand mabao 5-1. Cap Verde ilitoka sare ya kutofungana na Saudi Arabia, huku Uhispania ikipata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Uruguay.

Katika mechi nyingine za Ijumaa katika  Kombe la Dunia , Senegal waliiburuza Iraq kwa mabao 5-0 na Ufaransa ikiichapa Norway 4-1. Siku ya Jumamosi, Panama watashuka dimbani dhidi ya England huku Croatia ikimenyana na Ghana.

Hata hivyo timu za Afrika zapeta raundi ya 32 huku Ghana na Senegal zikiungana na mataifa mengine ya Afrika. Cape Verde itacheza na bingwa mtetezi Argentina, huku Afrika Kusini ikimenyana na Canada.  Morocco nayo itapambana na Uholanzi, huku Ivory Coast ikishuka dimbani dhidi ya Norway.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW