1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mechi za kufuzu CHAN 2025 zaendelea barani Afrika

23 Desemba 2024

Michuano ya kandanda ya kufuzu kwa Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) ambayo inawahusisha wachezaji wanaocheza ligi za ndani barani humo imeendelea katika viwanja mbalimbali usiku wa kuamkia leo.

Ghana
Ghana imetoka sare ya bila kufungana na NigeriaPicha: Metin Pala/AA/picture alliance

Michuano ya kandanda ya kufuzu kwa Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN)ambayo inawahusisha wachezaji wanaocheza ligi za ndani barani humo imeendelea katika viwanja mbalimbali usiku wa kuamkia leo.

 Nigeria imetoka sare ya 0-0 dhidi ya majirani zao Ghana. Wakati huo huo, mabingwa watetezi Senegal walichukua uongozi ambao ulidumu kwa dakika sita pekee katika sare ya 1-1 ugenini dhidi ya Liberia mjini Paynesville.

Soma zaidi.Ghana huenda ikashindwa kufuzu fainali ya Kombe la Mataifa Afrika 

Katika mchezo mwingine Ivory Coast walipata uongozi wa 2-0 dhidi ya Burkina Faso mjini Abidjan huku Sudan ikiivurumisha Ethiopia kwa magoli  2-0.

Michuano hiyo itafanyika mapema mwakani ambapo nchi za Tanzania,Kenya na Uganda zinayaandaa mashindano hayo kwa pamoja.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW