1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mechi za mzunguko kuwania kufuzu AFCON zaendelea

13 Oktoba 2024

Mechi za mzunguko za kuwania kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON zinaendelea.

Wachezaji wa timu ya Senegal na Ivory Coast wakipambana wakati wa mechi ya Afcon
Wachezaji wa timu ya Senegal na Ivory Coast wakipambana wakati wa mechi ya AfconPicha: Themba Hadebe/AP/picture alliance

Wakiwa nyumbani katika mji wa Oujda, Morocco iliigaragaza Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa mabao 5 kwa 0 huku Gabon ikitoka sare ya kutofungana na Lesotho. Siku ya Ijumaa, Comoro iliishangaza Tunisia kwa kuifunga bao 1-0 na hivyo kumaliza ubabe wa Tunisia wa ushindi mfululizo wa mechi 16 wakiwa nyumbani.

Soma pia: CAF: Michuano ya AFCON kuandaliwa mapema mwaka 2026

Mzunguuko wa nne unaanza hii leo Jumapili na mechi moja ambapo Burundi itamenyana na Burkina Faso. Mechi nane zitachezwa siku inayofuata na nyingine 15 siku ya Jumanne.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW