1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kuelekea mechi za nusu fainali za michuano ya AFCON

5 Februari 2024

Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON inaingia wiki hii katika hatua ya nusu fainali. Nigeria ilikuwa timu ya kwanza kutinga nusu fainali baada ya kupata ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Angola.

AFCON 2024
Kipa wa Afrika Kusini Ronwen Williams akiokoa mkwaju wa penaltiPicha: Samuel Shivambu/ BackpagePix/empics/picture alliance

Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON inaingia wiki hii katika hatua ya nusu fainali.

Nigeria ilikuwa timu ya kwanza kutinga nusu fainali baada ya kupata ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Angola huku Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ikinyakuwa ushindi kwa  kuikung'uta Guinea mabao 3-1.

Wenyeji Ivory Coast pia wamejikatia tiketi ya kucheza nusu fainali baada ya kupata ushindi wa 2-1 katika dakika za mwisho za muda wa ziada dhidi ya Mali. Ivory Coast sasa itachuana na Kongo katika mchezo wa nusu fainali.

Afrika Kusini,Bafana Bafana,  iliyoitowa  Cape Verde kupitia mikwaju ya Penalti baada ya kutoka sare ya bila kufungana sasa watakutana na mabingwa mara tatu wa AFCON Super Eagles Nigeria, mjini Bouake.

Mechi hizo za nusu fainali zitachezwa Jumatano, Februari 7.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW