Melbourne, Australia. Moto waharibu hekta kadha.
13 Desemba 2006Matangazo
Moto mkubwa umeharibu zaidi ya hekta 400,000 za misitu na maeneo ya kilimo kusini mashariki ya Australia. Kiasi ya wazimamoto 4,000 wanapambana na moto huo ambao bado unawaka ukiwa haujadhibitiwa katika jimbo la kusini la Victoria na Tasmania , licha ya kuwa hali ya hewa imekuwa ya wastani baada ya siku ya Jumapili joto kufikia kiwango cha centigrade 41.1, kiwango cha juu kabisa cha joto katika mwezi wa Desemba kwa muda wa nusu karne. Serikali ya jimbo la Victoria imeahidi dola za Australia milioni 27 zaidi katika juhudi za mapambano dhidi ya moto huo huku kukiwa na tahadhari kuwa moto huo unaweza kuendelea kuwaka kwa zaidi ya wiki kadha.