MELBOURNE : Maandamano yapinga utandawazi
18 Novemba 2006Matangazo
Waandamanaji wanaopinga utandawazi wamepambana na polisi katika mji wa Melbourne nchini Australia kupinga mkutano wa mawaziri wa fedha na magavana wa benki kuu kutoka nchi za kundi la mataifa 20 yenye maendeleo ya viwanda duniani.
Maafisa waandamizi wa Benki ya Dunia na wa Shirika la Fedha la Kimataifa ni miongoni mwa wanaohudhuria mkutano huo.
Maandamano ya kuupinga mkutano huo yamefanyika licha ya kuwepo kwa msako mkubwa wa usalama katika mitaa ilioko karibu na eneo la mkutano ambalo limefungwa kwa vizuizi vya barabarani pamoja na kufungwa kwa njia.