SiasaAsia
Meli iyozama zaidi ya miaka 80 yagundulika
22 Aprili 2023Matangazo
Timu ya inayoratibu zoezi la utafutaji na serikali ya Australia imesema imeyagundua mabaki ya meli iliyoshambuliwa na nyambizi ya Marekani miaka zaidi ya 80 iliyopita na kusababisha vifo vya takribani watu 1,060.Taarifa ya Wakfu wa Silentworld imesema mabaki ya meli hiyo ya usafirishaji ya Japan, iliyoshambuliwa katika kipindi cha Vita Vikuu Vya Pili vya Dunia- SS Montevideo Maru imekutwa katika eneo la bahari la Ufilipimo kwenye kina cha maji cha zaidi ya mita 4,000.Meli hiyo ya Kijapani ilikuwa ikiwasafirisha Waaustralia na raia wa mataifa mengine kadhaa hadi Kisiwa cha Hainan kutoka Rabaul, kwa sasa ukifahamika kama New Papua Guinea, baada ya eneo hilo lilikuwa katika mamlaka ya Australia kuangukia mikononi mwa Japan.