1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaYemen

Meli moja yashambuliwa nchini Yemen

28 Aprili 2023

Meli moja imeshambuliwa katika bahari kusini mwa Yemen, kwa mujibu wa shirika la Uingereza linaloshughulika na usafirishaji wa bidhaa kwa njia ya bahari, ambalo hutoa indhari ya kiusalama kwa meli za kibiashara.

China USA Kriegsschiff USS Milius Japan
Picha: Mass Communication Specialist 2nd Class Michael B. Jarmiolowski/U.S. Navy/abaca/picture alliance

Shirika hilo limesema meli hiyo ambayo haijatambuliwa imeshambuliwa kwa risasi katika Ghuba ya Aden. Hakuna taarifa zaidi zilizotolewa kuhusiana na shambulizi hilo.

Haya yanajiri siku moja tu baada ya Iran kuikamata meli moja ya mafuta iliyokuwa inaelekea Marekani katika Ghuba ya Oman. Iran inasema ilichukua hatua hiyo kwa kuwa meli hiyo ilihusika katika ajali iliyosababisha kupotea kwa wahudumu wawili wa meli.

Marekani imeitaka Iran iiachilie meli hiyo ikisema hatua hiyo inakwenda kinyume na sheria ya kimataifa na inatatiza usalama wa kikanda.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW