1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Meli nyingine ya mizigo yaondoka bandari ya Ukraine

2 Septemba 2023

Meli ya tatu ya mizigo itaondoka nchini Ukraine leo licha ya kuwepo vitisho vya Urusi karibu na eneo la bahari ya Bulgaria.

Ukraine | Das Getreideterminal im Hafen von Odessa
Usafirishaji bidhaa za Ukraine unaandamwa na wasiwasi wa hujuma tangu Moscow ilipojitoa kutoka mkataba wa kuruhusu Kyiv kusafirisha nafaka kupitia Bahari Nyeusi Picha: Bo Amstrup/Ritzau Scanpix/picture alliance

Eneo hilo linatumiwa kwa muda na meli zinazotoka bandari za Ukraine, tangu Moscow ilipojitoa kwenye mkataba wa kusafirisha nafaka na bidhaa nyingine za Ukraine.

Taarifa ya mipango ya safari ya meli hiyo zimetolewa na maafisa wa bandari nchini Ukraine, siku moja baada ya meli nyingine mbili za mizigo kung´oa nanga zikitumia ujia wa maji baina ya mataifa ya Romania na Bulgaria.

Meli mbili za kwanza zilizobeba maelfu ya tani za chuma ziliondoka kutoka bandari ya Yuzhny jana Ijumaa na zilitarajiwa kuwasili kwenye bandari ya Romania iliyo katika ukanda wa Bahari Nyeusi leo Jumamosi.

Safari za vyombo hivyo ilianza muda mfupi baada ya kuthibitishwa mkutano kati ya rais Vladimir Putin wa Urusi na mwenzake wa Uturuki Reccip Tayyip Erdogan utakaofanyika Jumatatu, ukilenga kuufufua mkataba wa usafirishaji nafaka za Ukraine.