1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Meli ya Ocean Viking yawaokoa wahamiaji zaidi ya 600

12 Agosti 2023

Meli ya hisani inayofanya operesheni za uokoaji kwenye bahari ya Mediterania ya Ocean Vking imewanusuru zaidi ya wahamiaji 600 katika kipindi cha saa 48 zilizopita.

Meli ya OCean Viking katika Bahari ya Mediterania
Meli ya OCean Viking katika Bahari ya MediteraniaPicha: Michael Bunel/Le Pictorium/IMAGO

Takwimu hizo zinaashiria ongezeko jipya la idadi ya watu wanaofanya safari hatari kujaribu kuingia Ulaya.

Soma zaidi: Italia kuwa mwenyeji wa mkutano wenye lengo la kupunguza wimbi la wahamiaji

Shirika linaloendesha meli hiyo la SOS Méditerranée limesema wengi wa waliookolewa walikuwa safarini kutoka mji wa mwambao wa Italia wa Sfax wakielkea kisawa cha Lampedusa nchini Italia.

Soma zaidi: Wahamiaji zaidi ya 900 wafa maji pwani ya Tunisia

Kulingana na shirika hilo jumla ya watu 623 waliokuwa wakisafiri kwa kutumia boti hatari za mpira wamepatiwa msaada na sasa wamo kwenye meli ya Ocean Viking na wanatarajiwa kufikishwa kwenye bandari za Italia baadaye leo.

Wahamiaji hao ni kutoka mataifa ya Sudan, Guinea, Burkina Faso, Ivory Coast, Benin na Bangladesh. Uokoaji huo umefanyika kiasi wiki moja tangu kutokea vifo vya makumi ya wahamiaji baada ya boti kadhaa kuzama baharini zikiwa njiani kuelekea mataifa ya Ulaya.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW