SiasaUrusi
Meli ya mizigo ya Urusi yazama baada ya kulipuka
25 Desemba 2024Matangazo
Taarifa hiyo imetolewa na wizara ya mambo ya nje ya Urusi. Wizara hiyo imeeleza kuwa chombo hicho kilizama baada ya kutokea mlipuko katika chumba cha injini. Wizara hiyo imesema wafanyakazi 14 kati ya 16 waliokolewa na kupelekwa katika bandari ya Uhispania ya Cartagena. Mmiliki wa meli hiyo ambayo ni wizara ya ulinzi, inayotoa pia huduma za kusafirisha abiria na vifaa, imesema meli hiyo, kwa jina Ursa, ilikuwa imebeba winchi za bandari na vifuniko vya vifaa vya meli vinavyotumika kuvunja barafu.