1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUrusi

Meli ya mizigo ya Urusi yazama katika bahari ya Mediterania

25 Desemba 2024

Wafanyikazi wawili hawajulikani walipo baada ya meli ya mizigo ya Urusi kuzama kwenye bahari ya Mediterania kutokana na mlipuko katika meli hiyo.

Moja ya meli ya mizigo ya Urusi
Moja ya meli ya mizigo ya UrusiPicha: Yoruk Isik/REUTERS

Taarifa hiyo imetolewa na wizara ya mambo ya nje ya Urusi. Wizara hiyo imeeleza kuwa chombo hicho kilizama baada ya kutokea mlipuko katika chumba cha injini.

Wizara hiyo imesema wafanyakazi 14 kati ya 16 waliokolewa na kupelekwa katika bandari ya Uhispania ya Cartagena.

Mmiliki wa meli hiyo ambayo ni wizara ya ulinzi, inayotoa pia  huduma za kusafirisha abiria na vifaa, imesema meli hiyo, kwa jina Ursa,  ilikuwa imebeba winchi za bandari na vifuniko vya vifaa vya meli vinavyotumika kuvunja barafu.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW