1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Melinda:Wezesha wanawake kuisaidia Afrika

23 Oktoba 2014

Licha ya uwepo wa fikra tofauti juu ya maendeleo kwa wanawake mfadhili Melinda Gates, anaamini ukitaka kuisaidia Afrika kwanza anza na wanawake kwa kuwa ni ufunguo katika kukuza uchumi na maendeleo Afrika

Burundi Landwirtschaft
Kilimo cha wanawake nchini BurundiPicha: picture-alliance/Ton Koene

Bi Melinda akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Paris hivi karibuni , kuhusu mradi wa kuchangisha fedha kwa ajili ya wanawake na wasichana alisema kuwawezesha wanawake ni miongoni mwa malengo yenye kipaumbele chenye nguvu katika taasisi ya Bill na Melinda Gates katika mkakati wa kuwasaidia watu katika nchi zinazoendelea kuwa huru katika nyanja ya afya, uzazi wa mpango na hali ngumu ya maamuzi kuhusu uchumi.

Hii ni kutokana na kuwa na ushahidi unaoonyesha wanawake barani Afrika , Asia na Amerika kusini wanauwezo mkubwa wa kuweka akiba ya fedha na kuirudisha katika matumizi ya familia kuliko wanaume wanavyofanya. Ambapo kuweka akiba huko kuna msaada kwa familia ya mwanamke na jamii kwa ujumla hali ambayo inashawishi kuwasaidia wanawake na wasichana katika maendeleo.Kama kuna haja ya kukuza uchumi barani Afrika ni lazima uanze na wanawake licha ya kuwa mengi yanasemwa kuhusu mahitaji ya kuwawezesha wanawake ikiwemo ya kuzingatia katika kupunguza idadi ya uzazi na kuongeza jitihada za afya ya uzazi ambayo ni mkakati wa pili kati ya nane wa maendeleo ya milenia uliowekwa mwaka 2000 na jitihada kubwa zimefanywa kulisogeza hilo mbele.

Melinda amefafanua kuwa vifo vinavyotokana na uzazi vimepungua mara tatu kwa miaka 30 iliyopita na vifo vya watoto wachanga vimepungua kwa nusu ya ilivyokuwa kabla ya mpango huu. Makundi ya misaada yanafanya kazi kwa mpango mpya wa Milenia wenye lengo la kukuza usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake ambako kutasaidia kupunguza umasikini na njaa.

Mwenyekiti mwenza wa taasisi ya Bill and Melinda GatesPicha: Getty Images

Kwa mujibu wa ripoti ya kilimo na chakula ya Umoja wa mataifa ya mwaka 2010 -2011, kama wanawake watashirikishwa katika kilimo kwa nchi zinazoendelea kutaongeza mazao na hatimae kutasaidia kupunguza idadi ya watu wanaokosa chakula kwa asilimia 12 mpaka 17.

Umuhimu wa kuwashirikisha wanawake katika kilimo

Kwa upande wa kukuza pato la taifa kwa asilimia 12 Gates anasema nia moja wapo ya kulifanikisha hilo ni kuwapa wanawake mbegu za mazao ya biashara ,kuwafundisha namna ya kupanda na namna ya kupata mbolea sahihi. Ila ni vyema kuhakikisha anapeleka mazao yake sokoni kwa sababu anaweza kukuambia pindi mumewe akiyapeleka sokoni ana wasiwasi wa kupewa kilichopatikana mkononi au kama watakubaliana hakuna kitachoenda sawa.

Hivyo ni lazima kuwajengea wanawake uwezo wa kushirikiana kwa kuwa wanawake sio tu ufunguo kwa ukuaji wa uchumi katika nchi zinazoendelea hata kwa nchi wanachama wa Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD) wanachokiangalia ni kama wanawake wameshirikishwa kikamilifu katika nyanja ya uchumi ili kukuza pato la taifa kwa asilimia 12.

Hata hivyo Mellinda anaamini kuongezeka kwa pato la taifa kutakako washirikisha wanawake kunaweza kufanikiwa barani Afrika na sio tu kudhibiti matumizi ya fedha bali pia kuwa na uzazi wa mpango, elimu na afya kama ulivyo mradi wa kurutubisha bidhaa zilizotumika katika kilimo kutengeneza pedi zinazotumiwa na wanawake katika siku zao za mwezi uliofadhiliwa na Taasisi ya Bill na Melinda Gets.

Hata hivyo Bi Mellinda amesema walicho kifanya mjini Paris ni kuionyesha serikali ya Ufaransa kuwa kuendelea kuwekeza kwa wanawake na wasichana ni muhimu sana kama tunataka maendeleo ulimwenguni. Sehemu ya bajeti ya Ufaransa inayotengwa kwa lengo maalum la msaada wa kimataifa imeporomoka kwa asilimia 3 mwaka 2015 hadi kufikia Euro bilioni 2.8 na inatarajiwa kushuka zaidi mwaka 2016 na 2017.

Mwandishi:Zuhura Hussein/AFP.
Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman.

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi