1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Meloni: Mashambulizi dhidi ya vikosi vya UNIFIL hayakubaliki

Sylvia Mwehozi
19 Oktoba 2024

Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni amesema mashambulizi dhidi ya vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa nchini Lebanon UNIFIL hayakukubaliki.

Giorgia Melon na Najib Mikati
Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni na mwenyeji wake waziri mkuu wa Lebanon Najib MikatiPicha: Hassan Ammar/AP Photo/picture alliance

Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni ameshutumu mashambulizi dhidi ya vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa nchini Lebanon UNIFIL akisema hayakukubaliki. Kiongozi huyo wa Italia ameyasema hayo wakati wa ziara ya nchini Lebanon.

Katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na Waziri Mkuu wa Lebanon Najib Mikati, Meloni alisema kuwa jukumu la UNIFIL katika kanda hiyo bado ni muhimu. Hayo yanajiri baada ya kikosi cha UNIFIL kudai kuwa kifaru cha Israel kilishambulia mojawapo ya kituo chake na kusababisha uharibifu wa vifaa.

Wakati huo huo jeshi la Israel IDF limesema kuwa litapeleka kikosi cha ziada cha askari wa akiba kwenye mpaka wake na Lebanon wakati kikipambana na Hezbollah. Kundi hilo nalo limenukuliwa hapo jana likisema linaingia katika awamu mpya katika vita vyake dhidi ya Israel.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW