1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merkel ajibu maswali ya wabunge kwa mara ya mwisho

Iddi Ssessanga
23 Juni 2021

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amewahimiza raia kuwa wangalifu, huku akisifu hatua za kudhibiti virusi vya corona na kuelezea matumaini ya ufufukaji wa kiuchumi wakati akijibu maswali ya wabunge kwa mara ya mwisho.

Berlin Angela Merkel Kabinettssitzung
Picha: Henning Schacht/Pool/Getty Images

Katika muda wa miezi mitatu kuelekea uchaguzi mkuu wa bunge, kutakuwa na idadi inayoongezeka ya ripoti kuhusu anachokifanya Angela Merkel, kukisema au kuamua jambo kwa mara ya mwisho.

Katika kipindi chake cha mwisho cha maswali na majibu bungeni siku ya Jumatano, kansela Merkel amesalia kuwa na utulivu wake uliozoeleka. Ametumia maneno ya wazi dhidi sheria ya mashoga nchini Hungary, hakuwa muwazi sana juu ya iwapo mwanamke anapaswa kuwa tena kansela.

Soma pia: Merkel: Hatua zilizoko sasa hazitoshi kudhibiti COVID-19

Lakini pia amejibu maswali kadhaa kuhusu mada nyingine, baadhi kwa namna ya kuchanganya.

Mwanzoni mwa kipindi chake cha kumi cha maswali na majibu katika muhula huu wa bunge, Merkel ameonesha mahitimisho chanya kuhusu usimamizi wa janga na covid-19.

Merkel akiaga baada ya kuhutubia siku ya viwanda ya Ujerumani inayoadhmishwa na chama cha wamiliki wa viwanda nchini humo, BDI.Picha: Bernd von Jutrczenka/dpa/picture alliance

Mafanikio dhidi ya janga la Covid-19

Amesema kwamba katika mawimbi yote matatu, malengo muhimu yamefikiwa na kuzuwia kuzidiwa kwa mfumo wa afya. Hali ya sasa ya maambukizo, Merkel ameitaja kama "ya kutia moyo." Hata hivyo janga bado halijaisha.

Akitazama nyuma mwaka mmoja na nusu wa janga, Merkel amazungumzia, "mafanikio makubwa katika historia yetu" na kusema Ujerumani imefanya mambo mengi sahihi, pia kwa kuilinganisha na mataifa mengine makubwa.

Soma pia: Merkel: Masharti magumu ni muhimu kudhititi COVID19

Lakini ameonya dhidi ya kuhatarisha mafanikio yaliopatikana tayari, na kuwahimiza raia kuendelea kuzingatia usafi. Ukweli kwamba wimbi la tatu limevunjwa, ilitokana na juhudi za jamii kwa ujumla, alisema.

Maswali ya wabunge yamezungukia kwenye mada za pensheni, tabianchi na sera ya kigeni hadi kwenye pango na kandanda.

Nafasi ya kansela mwingine mwanamke

Mbunge wa chama cha Kijani Ulle Schau alimuuliza Merkel iwapo ameridhishwa na mafanikio yaliofikiwa kwa wanawake katika nyanja ya siasa wakati wa muhula wake, na iwapo hangeunga mkono suala la mwanamke mwingine kuwa kansela.

Katika majibu yaliozusha kicheko kwa wabunge mbele ya mgombea mwanamke wa nafasi ya ukansela kutoka chama cha Kijani, Annalena Baerbock, Merkel amejibu kwamba baada ya miaka 16 ya Angela Merkel, raia ndiyo watakaoamua iwapo wanataka kansela mwanamke au mwanaume.

Merkel amejibu maswali ya wabunge mara tatu kwa mwaka wakati wa muhula wake. Hilo lilikuwa miongoni mwa makubaliano ya serikali ya muungano ya vyama vya CDU/CSU na SPD, kwamba kansela anakuja mwenyewe bungeni.

Mgombea ukansela kutoka chama cha Kijani Annalena Baerbock.Picha: Bernd von Jutrczenka/dpa/picture alliance

Hivi karibuni zaidi Merkel katika kikao chake cha maswali na majibu mnamo mwezi Machi, alikubali kubeba dhamana ya kuondoa vizuwizi vya Pasaka bungeni, na kuomba radhi kwa hilo.

Sheria ya mashoga Hungary

Wakati wa kikao chake cha mwisho, Merkel alitumia nafasi ya kujibu swali kutoka kwa mbunge wa chama cha AfD kukosoa vikali sheria ya Hungary dhidi ya mashoga. "Nadhani sheria hii siyo sahihi na pia haiendani na dhana yangu ya siasa," alisema.

Merkel amesema anaichukulia sheria hiyo kuwa kosa kwa mujibu wa uelewa wake wa siasa. Kiongozi huyo wa Ujerumani amesema anaona kama mkanganyiko, ukweli kwamba watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja wanakubalika nchini Hungary, lakini elimu kuwahusu inazuwiwa.

Chanzo: Mashirika