Merkel aonya juu ya changamoto zinazoikabili Ujerumani
5 Septemba 2017Akizungumza leo katika kikako cha mwisho cha bunge la shirikisha Bundestag, kabla ya uchaguzi mkuu wa Septemba 24, Merkel maeitolewa mwito Ulaya kuendelea kuwa na umoja dhidi ya uchokozi unaofanywa na rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, na kutoa mchango zaidi katika kukomesha mgogoro kuhusiana na mpango wa silaha za nyuklia wa Korea Kaskazini.
Merkel amesema Uturuki ilikuwa inatoka kwa kasi kwenye njia ya utawala wa sheria na kuapa kuwashinikiza washirika wa Ujerumani ndani ya Umoja wa Ulaya kutafakari juu ya kusitisha au kukomesha kabisaa mazungumzo ya nchi hiyo kujiunga na uanchama wa umoja huo, wakati wa mkutano wa kilele uliopangwa kufanyika mwezi ujao wa Oktoba.
Zikiwa zimesalia chini ya wiki tatu tu kabla ya uchaguzi, Merkel ameelezea kuvunjwa moyo na Uturuki, na kuzunguzia wazi nia yake mbele ya bunge, baada ya hapo Jumapili kutoa maneno makali zaidi, na kusema Uturuki haipaswi kuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya.
"Hakuna litakalostajaabisha zaidi kuliko kutofautiana hadharani, kuhusu uhusiano wa baadae na Uturuki tena machoni pa rais Erdogan. Hilo litadhoofisha vibaya nafasi ya Ulaya, naweza tu kushauri dhidi ya hilo," alisema Merkel mbele ya bunge mjini Berlin.
Merkel amelaazimisha kulizusha tena suala la kukomesha mazungumzo juu ya uachana wa Uturuki ndani ya Umoja wa Ulaya, baada ya mpinzani wake kutoka chama cha Kisoshalisti SPD Martin Schulz kusema wakati wa mdahalo wa Jumapili kati yao kwamba, ataachana na mazungumzo hayo ikiwa atashinda uchaguzi.
Tuhuma za Erdogan dhidi ya Ujerumani
Rais Erodan anaituhumu Ujerumani kwa kuwahifadhi wapangaji wa njama ya mapinduzi ilioshindwa mwaka 2016. Uturuki imewakamata karibu watu elfu 50 katika safisha safisah ya taasisi za serikali na vikosi vya ulinzi.
Ankara inasema ukandamizaji huo unalenga kuhakikisha usalama wa taifa lakini mataifa mengi ya magharibi na mashirika ya kutetea haki za binadamu yanasema ni jaribio la rais Erdogan kuzima upinzani. Erogan aliongezewa madaraka mapya katika kura ya maoni iliofanyika mwezi Aprili.
Licha ya nguvu ya sasa ya uchumi wa Ujerumani, Merkel amewaambia wabunge huu siyo wakati wa taifa hilo kulegeza kamba, akibainisha hasa changamoto zinazoikabili sekta iliyokumbwa na mgogoro ya magari, ambayo ndiyo muuzaji mkuu wa bidhaa za nje na ikiajiri karibu wafanyakazi 828,000.
"Sekta ya magari ni mmoja ya nguzo kuu za mafanikio ya kiuchumi ya Ujerumani. Lakini wafanyakazi wa sekta hii, ambao hawana kosa na wanafanya kazi zao vizuri sana, hivi sas a wako hatarini kwamba kupotea kwa imani katika uongozi wa makampuni ya mgari kuna athari kwao," alisema Merkel.
Mgogoro wa rais ya Korea
Baada ya kuzungumza na rais wa Korea Kusini Moon Jae In na rais wa Marekani Donald Trump, kujadili kitisho kinachowekwa na Korea Kaskazini, Merkel amewambia wabunge kwamba mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya watakutana nchini Ujerumani mwishoni mwa wiki hii.
Merkel na mpinzani wake mkuu katika uchaguzi wa septemba 24, Martin Schulz walitarajiwa kupambana tena katika mdahalo mbele ya wabunge, hii ikiwa ndiyo siku y mwisho ya muhula wa bunge hilo.
Mwandishi: Iddi Ssessanga/dpae,rtre
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman