1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merkel asema hatoshirikiana na wenye misimamo mikali.

30 Agosti 2017

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani katika maoni yao wanazungumzia juu ya hotuba ya mwaka ya kansela Angela Merkel kwa waandishi wa habari, kampeni za uchaguzi zinazoendelea na vilevile mgogoro wa wakimbizi.

Deutschland Wahlkampf CDU- Merkel in Bitterfeld
Picha: DW/K.-A. Scholz

Gazeti la Münchner Merkur limeandika kwamba kutokana na historia ya mikutano hii na waandishi wa habari, inashangaza kwamba Kansela Angela Merkel wa mwaka huu wa 2017 ni  kama yule yule wa 2013. Kila kitu kwa upande wake kinaonekana kuwa kawaida. Lakini kansela Merkel katika mkutano huo na waandishi wa habari alikwepa maswali muhimu kwa sababu ana mambo muhimu ya kufanya katika siasa za ulimwengu.

Merkel pia amesema hatoweza kushirikiana na vyama vyenye misimamo mikali ya mirengo ya kulia na kushoto, katika kuunda serikali yake ijayo. Kampeni ya Uchaguzi, ambayo inasisimua itatoa maamuzi katika uchaguzi wa tarehe 24 mwezi wa 9 ambapo kansela Merkel anasubiri kwa mara nyingine tena kuwa katika utawala. Juu ya kampeni za uchaguzi zinazoendelea mhariri wa gazeti la Stuttgarter Nachrichten anasema mgombea wa chama SPD Martin Schulz anajaribu yote katika kampeni yake lakini juhudi zake zinazidi kukatisha tamaa. Hata hivyo, tafiti za maoni zinaonyesha kuwa yuko  imara  kwa kiwango sawa na kansela Angela Merkel, binafsi Schulz haoni aibu kuendelea  ijapokuwa kampeni yake inaendelea kupoteza muelekeo. 

Mwenyekiti huyo wa SPD anataka kufikiwe makubaliano ya haraka juu ya malipo sawa kwa wastaafu wa iliyokuwa Ujerumani mashariki na magharibi pia anataka uwiano wa kitaifa katika masuala ya elimu. Schulz pia anataka kusitisha kodi itakayotozwa waendesha magari  hatua ambayo inaonekana kuwa haifai. Nae mhariri wa gazeti la Hannvorsche Allgemeine anazungumzia juu ya mgogoro wa wakimbizi, anasema ukweli usemwe na lazima nchi za Ulaya zitambue kwamba vijana wengi wa Afrika wanakimbia umasikini kutoka kwenye nchi zao na sio vita. Senegal, Nigeria na Cote di'voir hazikuwakilishwa kwenye mkutano wa mjini Paris. Naye mhariri wa gazeti la Neue Osnabrücker anasema nchi za Ulaya zimeshindwa katika sera ya wakimbizi. Mhariri huyo wa gazeti la Neue Osnabrückeranasema tatizo la wakimbizi halitotatuliwa kwa kushirikiana na zile nchi ambako wakimbizi hao wanapitia ni katika nchi ambazo wakimbizi hao wanatokea.

Mwandishi:Zainab Aziz/Münchner Merkur/Stuttgarter Nachrichten/Hannoverche Allgemeine/Neue Osnabrücker Zeitung.

Mhariri:Iddi Ssessanga

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW