Merkel asema milango itabaki wazi
28 Julai 2016Katika mkutano wake wa kila mwaka na waandishi habari leo, Merkel alisema , wakati akijibu maswali juu ya kwanini hajatembelea maeneo ya matukio ya mashambulizi , na kusema tu kwamba atahudhuria sala ya kumbukumbu siku ya Jumapili mjini Munich kwamba anaamini hatua alizochukua ni sahihi.
Merkel ambaye alikatisha likizo yake ya majira ya jotoili kuweza kuzungumza na vyombo vya habari mjini Berlin, leo,(28.07.2016) amesema mashambuliaji manne katika muda wa wiki moja , "yanashitua, yanadhalilisha na yanachosha" lakini sio ishara kwamba maafisa wamepoteza udhibiti.
"Ukweli kwamba watu wawili ambao waliingia nchini Ujerumani kama wakimbizi wanahusioka na mashambulio manne mjini Wurzburg na Ansbach wanaikejeli nchi iliyowachukua. Na ningependa kuongeza kwamba hakuna umuhimu kabisa , hata kama watu hawa wawili waliwasili pamoja na wakimbizi wengine wengi kabla ama baada ya Septemba 4 mwaka jana."
Wajerumani wataendelea kuwa tayari kuwapokea wageni
Kiongozi huyo wa Ujerumani amesema washambuliaji "walitaka kukandamiza hisia zetu za kijamii, uwazi wetu na kuwapo kwetu tayai kuwasaidia watu wenye shida."
Merkel alikuwa akizungumza baada ya shambulio la shoka, visu, mashambulizi ya risasi na shambulio la kujitoa muhanga kuiacha Ujerumani katika bumbuazi , na kusababisha watu 13 , ikiwa ni pamoja na washambuliaji hao kufariki na wengine darzeni kadhaa kujeruhiwa.
"Sheria ya juu kabisa ni kwamba panapotokea mgawanyiko, ni lazima tuchukua hatua kama tulivyokwisha fanya hadi sasa, ili iwe wazi kwamba tutafanya kila linalowezekana kibinadamu kuhakikisha usalama katika taifa letu huru na la kidemokrasia."
Merkel ameongeza kwamba hataruhusu wapiganaji wa Jihadi , kufuatia mashambulizi kadhaa yaliyosababisha maafa , nchini Ufaransa, Ubelgiji, Uturuki na katika jimbo la Marekani la Florida pamoja na Ujerumani , kuiweka serikali yake kushindwa kuongozwa na sababu za msingi pamoja na uelewa.
Wakati tabaka la kisiasa nchini Ujerumani limetoa wito kwa kiasi kikubwa kuwa na utulivu, vyama vya upinzani na waasi kutoka katika kundi la kisiasa la kihafidhina vimemshutumu kwa kuiweka wazi nchi hiyo kuwa katika hatari ya kushambuliwa bila ya kuwa na udhibiti imara wa watu wanaoingia.
Mashambulio nchini Ujerumani yamefanyika wakati uchaguzi katika majimbo mawili unakaribia mwezi Septemba, mjini Berlin na Mecklenburg magharibi.
Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe / dpae
Mhariri: Josephat Charo