1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merkel asherehekea miaka 65 ya kuzaliwa

Sekione Kitojo
17 Julai 2019

Kansela Angela Merkel alianza mikutano ya baraza  la mawaziri mjini  Berlin leo kama  anavyofanya  siku  zote, ila pale alipopewa shada kubwa  la maua kwa kutimiza miaka 65 ya kuzaliwa.

Deutschland Bundeskanzlerien Angela Merkel bekommt Blumen zum Geburtstag
Picha: Getty Images/S. Gallup

Hatarajiwi kwenda umbali huo tena katika  maisha  yake  "Hii  ina maana huwezi  kuwa  kijana  tena. Lakini  huenda  suala la uzoefu  zaidi," Merkel  amesema  wiki iliyopita  wakati akiulizwa  kuhusu  siku  yake  ya  kuzaliwa. Leo  ni  siku  ya  kuzaliwa kwa  bibi  Merkel kuna  mengi  ya  kuzungumzia  kuhusu  miaka  65 ya  maisha  yake  na  kile  kinachofuata.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel Picha: picture-alliance/dpa/R. Jensen

Kansela  alizaliwa  mnamo  Julai 17 , 1954. Amekuwa  kansela  wa Ujerumani  mwaka  2005, kimsingi  akifanya  mabadiliko  makubwa nchini. Mara  kadhaa  akisifiwa  kwa  utulivu  wake , muda  wake madarakani  mara  nyingi  umekuwa  na  mitikisiko  mingi. Waziri wa kilimo  Julia Kloeckner  alimtakia  kansela siku  njema  ya  kuzaliwa kwake  kabla  ya  mkutano  wa  baraza  la  mawaziri , akimwita "mtu mwerevu, mwenye busara, mfuasi wa  nadharia  za  vitendo  na mwenye  uwezo  wa  kuwa  na  mwekeleo unaolenga  masuala makubwa, huyo  ni  Angela  Merkel.

Anasherehekea  siku  yake  ya  kuzaliwa  kama  ilivyotarajiwa, ameongeza  Kloeckner, "bila  ya  shauku  na  akifanyakazi."

Waziri wa kilimo Julia KloecknerPicha: picture-alliance/dpa/W. Kumm

Merkel  ambaye amesema  anataka  kuendelea  kuwa  kansela  hadi muhula  wake  utakapomalizika  mwaka 2021, hivi  karibuni amekuwa  akiketi  kitini  katika  shughuli  za  sherehe  za  kiserikali. Kutetemeka  kulianza  kuonekana  katikati  ya  mwezi  Juni  katika mapokezi  ya  waziri  mkuu  mpya  wa  Ukraine Volodymyr Zelensky.

Kutetema

Merkel  alisema  wakati  huo  kuwa  alikuwa  ameishiwa  maji  mwilini katika  siku  ambayo  ilikuwa  na  joto  kali. Matukio  mengine  ya kutetemeka  yalielezwa  kuwa  ni mchakato  wa  kisaikolojia  wa tetemeko  la  kwanza. Madaktari  hawakuwa tayari kuelezea mawazo yao  kuhusu  afya  ya  Merkel, ambayo  inaelezewa  kuwa  ni  suala la  binafsi nchini  Ujerumani, hata  kama  ni  kiongozi. Lakini binafsi bibi  Merkel  leo  alisema:

"Najisia  vizuri. Nimesema  hivi  karibuni  kuwa  nafanyia  kazi  kile kilichonitokea katika  wakati  wa  gwaride  la  jeshi  na  waziri  mkuu wa  Ukraine Volodymyr Zelenskiy. Hatua  hii  bila  shaka haijamalizika  lakini  kuna  hatua  imepigwa  na ninalazimika  kuishi na hali  hii  kwa  muda  lakini hali  yangu  ni  nzuri  na  hamna sababu ya kuwa na  wasi  wasi juu  yangu."

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky (kushoto)Picha: AFP/S. Supinsky

Rais  wa  Urusi  Vladimr  Putin  amempongeza  Merkel  katika  siku yake  ya  kuzaliwa  kwa  ujumbe  ambao  unatoa  sifa  kwa  uongozi wake pamoja  na  miaka  kadhaa  ya  mafanikio kama  kansela.

Merkel  ambaye  amekuwa  kansela  tangu  mwaka  2005 , ameendelea kuwa kiongozi  anayependelewa  na  watu  kwa kiwango cha  juu  hata pale  chama  chake  cha  Christian Democratic Union CDU  kimepata kuporomoka  katika  maoni  ya wapiga  kura, ambapo inaonesha  chama  cha  walinzi  wa  mazingira kikionekana  kupanda  katika  umaarufu.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW