Matokeo ya awali yampa Merkel ushindi
24 Septemba 2017Kansela Angela Merkel anaonekana kuumizwa kwenye uchaguzi huu kwa kupoteza asimilia kadhaa, lakini bado ndiye mwenye nafasi ya kuongoza muhula wa tatu wa ukansela.
Lakini nani atamchukuwa kuwa mshirika wake kwenye serikali ya mseto?
Tayari mgombea wa Social Democrat (SPD), Martin Schulz, ametangaza kukubali kushindwa lakini akiweka wazi kuwa hatajiunga na serikali ya mseto, na badala yake ataongoza upinzani.
SPD imepoteza asilimia 5.3 kulinganisha na ushindi wake wa awali, huku chama cha siasa kali za mrengo wa kulia, AfD, kikiongeza asilimia 8.3 kwenye bunge la shirikisho, Bundestag.
Kansela Merkel amesema kwamba alitazamia ushindi mkubwa zaidi, lakini wapigakura wameamua kuwa Ujerumani inapaswa kuongozwa kwa ushirikiano wa vyama. Na sasa kinachosubiriwa ni muungano upi utaongoza.
Zaidi angalia hapa: http://www.dw.com/sw/idhaa-ya-kiswahili/s-11588