1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela Merkel awasili katika Ikulu ya Marekani

15 Julai 2021

Rais Joe Biden wa Marekani amemkaribisha Kansela Angela Merkel wa Ujerumani katika ikulu ya White House, kwa kile kinachoonekana kuwa ziara yake ya mwisho rasmi iliyobeba ujumbe mzito wa Ujerumani.

USA l Bundeskanzlerin Merkel trifft Vize-Präsidentin Harris
Picha: Andrew Harnik/AP/picture alliance

Pamoja na mengine mengi, kiongozi huyo mkongwe wa Ujerumani leo hii anatarajiwa kuweka mezani mambo kadhaa ukiwemo mjadala kuhusu kuinukia kwa China na juu ya mradi wa bomba la gesi kutoka Urusi hadi barani Ulaya ambao unapingwa na Marekani. Mijadala mingine ni mabadiliko ya tabia nchi, usaambazaji wa chanjo ya Covid-19 pamoja na hatma ya Afghanistan kwa sasa katika kipindi hiki ambacho vikosi vya Marekani, Ujerumani na mataifa mengine vikiondoka katika ardhi ya taifa hilo.

Katika ziara hiyo Kansela Merkel atafanya mazungumzo pia na makamu wa rais Kamala Harris na viongozi waandamizi wengine wa Marekani kabla ya mazungumzo yake ya ana kwa ana na Rais Biden.

Merkel kutunukiwa shahada ya heshima ya falsafa.

Baada ya mkutano wao wa mchana Biden na ujumbe wake Ikulu watafanya mkutano na waandishi wa habari na kisha rais amepanga kuandaa chakula cha jioni kwa ajili ya kuonesha heshma kwa Bi. Merkel na mume wake Joachim Sauer. Lakini pia Merkel atatunukiwa shahada ya heshma ya farsafa18 kutoka chuo kikuu cha Johns Hopkins ambapo pia imepangiwa kukihutubia chuo hicho.

Afisa mwandamizi kutoka taasisi ya Kijerumani inayojihsisha na masuala ya kimataifa na mahusiano ya kiusalama yenye maskani yake mjini Berlini, Johannes Thimm amesema katika ziara yake hiyo ambayo ni ya kuaga Merkel atawasilisha ujumbe wa uhusiano madhubuti baina ya Ujerumani na Marekani. Baada ya miaka 16 ya kufanya kazi na Merkel, idadi kubwa ya maafisa wa serikali ya Marekani na mataifa mengine wanajiuliza ni mkondo gani Ujerumani itachukuwa baada ya uchaguzi ujao wa taifa hilo, amsema Thimm.

Chama cha Merkel CDU, kinaongoza katika kura ya maoni kabla ya uchaguzi mkuu wa Septemba 26, lakini kile cha watetezi wa mazingira cha The Green na cha siasa za wastani za mrengo wa shoto Social Democrats SPD, pia vinapigania kuongoza serikali ijayo ya Ujerumani.

Chanzo: APE/AFP

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW