1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merkel azishambulia Marekani na Uingereza

30 Januari 2014

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ameonya leo(29.01.2014)kuwa nchi zinazofanya ujasusi kwa washirika wake wanahatarisha kuvunja uaminnifu, na kusababisha hali ambayo si salama badala ya kuimarisha usalama.

Angela Merkel Regierungserklärung 29.01.2014
Kansela Angela MerkelPicha: Reuters

Merkel ameyasema hayo katika hotuba yake baada ya kuapishwa rasmi kuchuguliwa tena kuiongoza serikali ya mseto kwa kipindi kingine cha tatu.

Merkel alitumia hotuba hiyo kuzishambulia Marekani na Uingereza kuhusiana na mipango yao ya ujasusi. Miongoni mwa madai yaliyojitokeza kutokana na nyaraka za siri za serikali ya Marekani zilizovujishwa na mfanyakazi wa zamani wa shirika la usalama wa taifa la Marekani Edward Snowden mwaka jana ni kwamba mataifa rafiki pamoja na viongozi wao , ikiwa ni pamoja na Merkel wamekuwa lengo la udukuzi.

Bunge la UjerumaniPicha: picture-alliance/dpa

Marekani imesema kuwa mipango yake ya upelelezi ina lenga katika kitisho kwa usalama wa taifa hilo, ikiwa ni pamoja na ugaidi.

Kuvunja uaminifu

"Vitendo mahali ambapo mbinu zinahalalisha matendo, wakati kila kitu ambacho kinawezekana kiufundi kinatumiwa, vinahatarisha hali ya kuaminiana," Merkel amesema.

"Inaonesha hali ya kutoaminiana. Hatimaye kunakuwa na hakuna usalama kabisa."

Kiongozi huyo wa Ujerumani amesema serikali yake inahisi umihumi wa kulinda haki ya faragha ya raia wake, pia. Lakini amekataa miito ya kuiwekea mbinyo Marekani ili kutia saini makubaliano ya kutofanya ujasusi kati ya nchi hizo mbili kwa kusitisha mazungumzo ya kibiashara kati ya Marekani na Umoja wa Ulaya.

"Naongoza mazungumzo haya kwa nguvu ya hoja zetu," amesema . " Nafikiri tuna hoja nzuri."

Amedokeza kuwa hatarajii kupata suluhisho lolote la rahisi, akisema , "ni njia ndefe mbele yetu."

Merkel pia amesema licha ya msuguano uliopo hivi sasa , "ushirika wa mataifa ya bahari ya Atlantic unaendelea kuwa muhimu sana."

Gregor Gysi kiongozi wa chama cha Die LinkePicha: Getty Images

"Ujerumani haiwezi kuomba kuwa na mshirika mzuri zaidi ya Marekani," amesema.

Akosolewa

Matamshi hayo yamesababisha ukosoaji kutoka kwa kiongozi wa chama cha upinzani cha Die Linke Gregor Gysi kwa kile alichosema " kupiga kwake magoti kwa Marekani."

Merkel amekubali mwaliko kutoka kwa rais Barack Obama kuitembelea Marekani katika miezi inayokuja, licha ya kuwa hakuna tarehe iliyokwisha pangwa hadi sasa. Msemaji wake Steffen Seibert amewaambia waandishi habari leo kuwa suala la udukuzi litajadiliwa katika ziara hiyo.

Msemaji wa kansela wa Ujerumani Steffen SeibertPicha: picture-alliance/dpa

Kuhusu masuala ya ndani Merkel ameapa kuweka msukumo wa kupandisha mishahara kwa wafanyakazi wanaopata kipato cha chini na kuimarisha mafao ya uzeeni kwa wazee katika muda wa miaka minne ijayo pamoja na kuweka sheria ngumu kwa masoko ya fedha. Amesema kuwa Ujerumani itaweka mshahara wa kima chini cha euro 8.50 kwa saa kuanzia mwaka ujao.

Mwandishi: Sekione Kitojo / ape / afpe

Mhariri : Mohammed Abdul Rahman

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW