Merkel kuzuru mataifa matatu ya Afrika
9 Oktoba 2016Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ametoa wito wa kuwa hali bora zaidi kwa uwekezaji wa binafsi katika mataifa ya Afrika ili kuweza kupambana na sababu zinazopelekea uhamiaji wa kiuchumi. Amssema hayo kabla ya ziara yake ya siku tatu katika mataifa ya Afrika inayoanza Jumapili(09.10.2016).
Ujerumani ina lenga kurejesha uhusiano wake na bara la Afrika baada ya mzozo wa wakimbizi. Sehemu ya mpango huo ni kutuma vikosi vya jeshi la Ujerumani kusaidia kuweka uthabiti katika bara hilo.
Kansela Angela Merkel ni kiongozi wa kwanza wa serikali ya Ujerumani kwenda mali. Niger na Ethiopia pia zimo katika orodha ya nchi atakazofanya ziara hiyo ya siku tazu, kuanzia mwishoni mwa juma hili.
Katika hali ya kushitua inayotanabahisha kuhusu hali tete katika eneo hilo, wanajeshi 22 waliuwawa na watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa jihadi nchini Niger siku ya Alhamis. Shambulio hilo lilifanywa dhidi ya kambi inayowahifadhi wakimbizi wa mali ambao wamewakimbia wanagambo wa Kiislamu nchini mwao.
Wakati ziara yake ikikaribia , kiongozi huyo wa Ujerumani amesisitiza kwamba uthabiti wa Umoja wa Ulaya unategemea sana kasi ya maendeleo katika bara la Afrika. Misaada zaidi ya maendeleo inahitajika, sera mpya ya maendeleo ni muhumu, uwekezaji katika bara hilo unahitajika kuongezwa na msisitizo mkubwa uwekwe katika utawala bora, Merkel amesema. Alikuwa akitoa hotuba katika chama cha wauzaji wa jumla na wasafirishaji nje bidhaa nchini Ujerumani mjini Berlin.
"Kwa ujumla , tunalazimika kuweka mtazamo wetu katika bara la Afrika katika njia mpya na tofauti," kansela alisema.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier aliitembelea Mali na Niger mwezi Mei mwaka huu. Nchi hizo zote mbili ni sehemu ya kituo cha kupitia wakimbizi wengi kutoka mataifa yao ya Afrika magharibi wakitafuta kufika Ulaya.
Niger na Mali zinakabiliwa na changamoto ya ugaidi wa kimataifa.
Vikundi vya kigaidi , kama al-Qaeda, vinagharamia shughuli zao kwa fedha kutokana na utekaji nyara na biashara ya madawa ya kulevywa katika eneo hilo la Sahara.
Baada ya mapinduzi ya kijeshi nchini Mali mwaka 2012, mamia kwa maelfu ya watu walikimbia makaazi yao kwasababu ya kutokuwa na uthabiti , ukosefu wa usalama na ukosefu wa njia sahihi za kupata chakula na maji safi ya kunywa. Katika nchi jirani ya Niger , magaidi wa kundi la Boko Haram, kundi la wanamgambo lililoko katika nchi jirani ya Nigeria, limekuwa na harakati, ambazo zimesababisha kuharibika kwa usalama katika nchi hiyo.
Haja ya uhamiaji
Denis Tull kutoka taasisi ya Ujerumani kwa ajili ya masuala ya kimataifa na usalama iliyoko mjini Berlin ililiambia shirika la habari la DW kwamba wahamiaji kutoka Afrika kupitia bahari ya Mediterania ni suala la umihumu mkubwa kwa Ujerumani. "Katika nchi kama Mali ama Senegal, uhamiaji ni jambo la kawaida, ni suala la utamaduni wa jamii, ikiwa ni sehemu ya utambulisho wa mtu na makuzi yake," amesema . Ni kitu ambacho kinaweza tu kuzuiwa kwa taabu kubwa. Tofauti kati ya eneo la kaskazini mwa Afrika, Sahel na Ulaya ni kubwa mno kwamba haja ya kuhamia haitapotea. " aliongeza. Misaada ya maendeleo haitasababisha kufutika kwa uhamiaji. Njia bora inayoweza kufikiwa inaweza kuwa uimarishaji wa ushirikiano wa hivi sasa kati ya mataifa.
Hii itaonekana kuwa kile Merkel alichonacho katika mawazo yake. Anataka kupanua miradi iliyopo ya maendeleo, kusaidia juhudi za kujenga miundo mbinu , kuwapa mafunzo na utengenezaji wa nafasi za ajira, kwa mujibu wa taarifa kutoka katika ofisi ya kansela.
Hata ongozana na ujumbe wa biashara. "Kwa kuwa hatuna maslahi ya kiuchumi na Mali, tutaangalia njia nyingine ya ushirikiano. Kiwango cha biashara na Mali ni kidogo mno," Merkel amesema.
Kuhusika kwa Ujerumani kijeshi kunaweza kusaidia kuleta uthabiti katika eneo la Sahel , Tull alisema. Ujerumani ina lenga kujenga kituo chake cha jeshi nchini niger, ambacho kitatoa msaada kwa MINUSMA, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Mali. Vikosi vya jeshi la Ujerumani tayari vinashiriki katika ujumbe wa MINUSMA pamoja na ujumbe wa kutoa mafunzo ya kijeshi wa Umoja wa Ulaya (EUTM). Merkel atafanya mikutano na vikosi vya Ujerumani katika uwanja wa ndege wa Mali , Bamako.
"Upanuzi wa shughuli za kijeshi za Ujerumani katika eneo la Sahel ni hatua moja mbele kwa Ujerumani wakati ikijaribu kujiweka katika nafasi kwa njia mpya katika bara la Afrika," alisema Oswald Padonou kutoka wakfu wa Konrad Adenauer. Yuko katika ofisi ya kanda ya taasisi hiyo inayojaribu kukusanya mawazo ya Ujerumani mjini Abidjan , Cote d'Ivoire, ambako anaendelesha mipango ya usalama na utawala bora katika Afrika kusini mwa jangwa la Sahara. Ujerumani ilikuwa imejiweka pembezoni kwa muda mrefu.
Lakini Ujerumani yenye uchumi mkubwa barani Ulaya, ikiwa na nia ya kuwa ujumbe wa kudumu katika baraza la Usalama la Umoja wa mataifa, haiwezi kuendelea kuwa katika hali kama hiyo tena. "Ujerumani ni lazima iwe na uwezo kuweka msimamo wake katika masuala ya siasa za dunia, hususan katika bara la Afrika, ambako masuala ya usalama ni muhimu," Padonou amesema.
Kituo cha mwisho katika ziara ya Merkel ni Ethiopia. Hii ni nchi ambayo imekosolewa sana kwasababu ya ukiukaji wa haki za binadamu. Mjini Addis Ababa , Merkel , atafungua jengo jipya la Umoja wa Afrika lililojengwa kwa fedha kutoka Ujerumani. Pia anataka kupata hisia ya hali ilivyo katika nchi hiyo binafsi kwa kuzungumza na maafisa wa serikali na wawakilishi wa vyama vya kijamii.
Katika maandamano ya Waethiopia wanaoishi nchini Ujerumani katika mji mkuu Berlin, mmoja wa washiriki wa maandamano hayo alimtolea wito kansela kuchukua ujumbe wake wa maandamano na kuuwakilisha Ethiopia na kuweka mbinyo kwa serikali ya nchi hiyo. " Watu wanakufa kila siku kule. Lakini wanapambana , kwa maandamano na kuweka vizuwizi. Siku ambapo watu watatauwawa kwa kupigwa risasi hovyo zimekwisha," alisema. Hii ni hali ambayo Ethiopia ni lazima itambue. "Serikali ya Ethiopia haiwezi kubembelezwa tena."
Mwandishi : Sekione Kitojo / zr /DPA
Mhariri: Sudi Mnette