1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merkel : "Sisi ni wananchi"

14 Januari 2017

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amewataka Wajerumani kutetea kwa nguvu maadili yanayofungamana na demokrasia na uhuru wakati nchi ikikabiliwa na ongezeko la sera kali za mrengo wa kulia na uchaguzi mkuu.

Deutschland Auftakt Klausurtagung CDU-Bundesvorstand
Picha: picture-alliance/dpa/O. Dietze

Katika mkutano wa chama chake katika mji wa Sarlouis Kansela ametaja makundi ya vuguguvu ya kiraia yenye chuki dhidi ya wageni kama vile PEGIDA  hayana haki ya kuamuwa nani anapaswa kustahiki kuwepo Ujerumani na nani astahiki upendeleo huo.

Akijitenganisha na wafuasi wa PEGIDA bila ya kulitajua kundi hilo kwa jina katika hotuba yake Merkel amesema :"Sisi sote ni wananchi" akiweka mstari kati yake na mahasimu wake wa sera kali za mrengo wa kulia ambao mara nyingi hutumia kauli  mbiu hiyo "sisi ndio wananchi "kujipatia umashuhuri.

PEGIDA ina wafuasi wengi sehemu za mashiariki mwa Ujerumani ambayo ilikuwa ikijulikana kama Jamhuri ya Kidemokrasi ya Ujerumani (GDR) hadi mwaka 1990.Kundi hilo limeichukuwa kauli mbii hiyo ya  "Sisi ndio wananchi "  kutoka maandamano ya kupinga ukomunisti ambayo yalikuwa yakifanyika kila Jumatatu katika makanisa mwishoni mwa miaka ya 1980 katika nchi nzima iliokuwa ikijulikana wakati huo kama GDR hususan katika mji wa Leipzig.

Merkel ana ufasaha wa kusema 

Kansela Angela Merkel.Picha: picture-alliance-dpa/O. Dietze

Baba wa Merkel alikuwa mchungaji katika kanisa moja Ujeumani mashariki jambo ambalo limewacha alama katika makuzi yake halikadhalika katika uongozi wake wa kisiasa.

Licha ya kuongezeka kwa uungaji mkono wa sera kali za mrengo wa kulia chama cha Merkel kinaongoza katika uchunguzi wa maoni kwa asilimia 37 ya kura.

Kiongozi huyo wa muda mrefu wa Ujerumani pia ameirudisha tena kauli mbiu nyengine ya kihistoria. Ameifuta vumbi kauli mbiu ya kisiasa iliokuwa ikitumika katika siku za awali za Ujerumani baada ya vita akisistiza kwamba "Ustawi kwa wote"itakuwa kauli mbiu yake kuu katika kampeni wakati Ujerumani ikijiandaaa kufanya uchaguzi mkuu baadae mwaka huu.

Katika miaka ya 1950 waziri wa kwanza wa uchumi wa Ujerumani baada ya vita Ludwig Erhard alichukuwa hatua za mfululizo za mageuzi ya kiuchumi chini ya beramu "Ustawi kwa wote". Mageuzi haya baadae yalipelekea kile kilichokuja kujulikana kama " Wirtshaftswunder" ikimaanisha " mijujiza ya kiuchumi".

"Tunaka watu wengi kadri inavyowezekana kuwa na ajira na malipo ya haki"amesema Merkel na kuongeza kwamba pia anataka makampuni yaendeshe shughuli zake chini ya mazingira ambayo yatarahisisha uwekezaji nchini Ujerumani na sio mahala kwengineko.

Haki za binaadamu zisichukuliwe kijuujuu

Kwa mujibu wa uchunguzi wa maoni chama cha Merkel cha CDU kinaongoza kwa asilimia 37 licha ya kuzidi kuungwa mkono kwa sera kali za mrengo wa kulia.Picha: picture-alliance/dpa/O. Dietze

Katika hotuba yake Kansela pia amesisitiza kwamba haki za binadaamu kama vile uhuru wa kuzungumza,dini na ule wa kujieleza kamwe haupaswi kuchukuliwa kuwa hauna masharti. Merkel amesema maadili sio "zawadi ambazo huzitakiwi kuzifanyia kazi."

Merkel ameongeza kusema inabidi kila mara wananchi waonyeshe juhudi na kuthibitisha kwamba watasimama kuutetea uhuru inapobidi.

Hata hivyo kauli yake hiyo huenda imkaishia katika masikio ya kufa ya wapiga kura wengi ambao wanasema lengo ni kuepuka kile kinachodaiwa kuwa mwenendo unaoendelea wa kukwama kwa uchumi na taathira hasi ambayo inaweza kusababishwa na utandawazi badala ya kulenga maadili na uhuru wa kiraia.

Mwandishi : Mohamed Dahman/DW/dpa

Mhariri: Isaac Gamba