1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merkel: "Tuko imara kuliko ugaidi"

Sekione Kitojo
31 Desemba 2016

Katika hotuba ya mwaka mpya, kansela wa Ujerumani Angela Merkel amewatolea wito raia kuuanza mwaka 2017 kwa matumaini na kupinga ugaidi. Lakini wahakikishe"usalama katika uhuru,"amesema hatua mpya huenda ni muhimu.

Deustchland | Neujahrsansprache BK Merkel im Bundeskanzleramt
Kansela Angela Merkel wa UjerumaniPicha: REUTERS/M. Schreiber

Mwaka  2016  unakaribia  kumalizika , na  mwaka  2017 unakaribia  kuingia nchini  Ujerumani. Katika  hotuba  yake  ya  mwaka  mpya , kansela  Angela Merkel  alisema  kwamba  miezi  12  iliyopita "ilikuwa  mtihani  mkubwa  kwetu katika  njia  nyingi." Miongoni  mwa  hizo , ugaidi  wa  itikadi  kali  ya Waislamu , "bisha shaka " ndio " mtihani  mkubwa mgumu." Nchi  ilishuhudia mlolongo  wa  mashambulizi  kwa  mwaka  mzima: Mjini  Würzburg, Ansbach na  hivi  karibuni  kabisa , Berlin.

watu  12 waliuwawa  wakati  Anis Amri alipoendesha  lori  katika  kundi  la watu  katika  soko  la  krismass  katika  mji  mkuu  wa  Ujerumani  Berlin Desemba 19. Mtunisia  huyo  mwenye  umri  wa  miaka  23  alikuja Ujerumani  kama  mkimbizi.

Ni "kitu  kichungu - na  kisichopendeza,"  alisema  kansela , wakati mashambulizi  ya  kigaidi  yanafanywa  na  watu "ambao  wamekuja  hususan kutafuta  hifadhi , mahali  salama  na  tena  wamepata  msaada." Vitendo  hivi "vinabeza" kuwapo  tayari  kwa  Wajerumani  kutoa  msaada , na  pia  kwa wale  watu " ambao wanahitaji  kweli  msaada  na  wanastahili ulinzi."

Kuwapo na nia thabiti

Kama  kawaida , majonzi  kuhusiana  na  waliouwawa  na  waliojeruhiwa  ni makubwa. Hii  ilionekana  katika  hotuba  ya  Merkel. Katikati  ya  maafa  kama hayo , Merkel alitoa  wito  wa  kujiamini "katika mtazamo  imara  wa  kusimama imara  dhidi  ya  dunia  ya  chuki  ya  magaidi  kwa  ubinadamu  wetu  na mshikamano."

Kansela Merkel akiweka shada la maua eneo lilipofanyika shambulio katika soko la Krismass mjini BerlinPicha: Reuters/H. Hanschke

Kwa  hakika , kansela  na  kiongozi  wa  chama  cha  kihafidhina  cha Christian Democratic Union CDU, wamethibitisha  msimamo  wake kuhusiana  na  sera  ya  wakimbizi  katika  ujumbe  wake  kwa  ajili  ya  mwaka mpya. "Na wakati  tunakabiliwa  na  picha  za  mji  uliopigwa  mabomu  wa Aleppo  nchini  Syria , tunasisitiza   kwamba  ni  muhimu  kiasi8  gani  na muhimu  kwa  nchi  yetu  kuwachukua  wale  ambao  kwa  kweli  wanahitaji msaada  wa  ulinzi, na kuwasaidia  kuweza  kujumuika hapa."

Kwa  kansela , magaidi  wanaishi  katika "dunia  iliyojaa  chuki"  na utawala  wa sheria  na  demokrasia  vinakwenda  kinyume  na hivyo. "Tuko  imara wakati tutakapojiunga  pamoja. Nchi  yetu  ni  imara," alisema,  na  kuongeza kwamba  taifa  ni  lazima  pia  lipambane  na  ugaidi  ili  kuweza  kuhakikisha "usalama  na  uhuru"  kwa  raia  wake. "Katika  mwaka  ujao , kama  itakuwa lazima, serikali  ya  Ujerumani  haraka  itaanzisha  na  kuidhinisha  sheria  ya ziada  na  hatua  za  kisera,"  alisema  Merkel.

Kuiokoa  demokrasia na  watu

Kansela  ameelezea  nia  yake  ya  kuwa  na  umoja  zaidi  na  kuimarisha demokrasia  katika  mwaka  mpya. Watu  wengi , alisema , watauhusisha mwaka  2016  na  hisia  kwamba  dunia ilipinduliwa  chini  juu. Mafanikio kama  Umoja  wa  ulaya  na  demokrasia  ya  bunge  vilipata  changamoto kwasababu  vionekana  kutojihusisha  na  maslahi  ya  raia.

"Lakini hii  ni  picha potofu,"  alisema  Merkel . Ndio , Ulaya  inaburuza  miguu , alisema Merkel, "lakini  sisi  Wajerumani  hatupaswi  kuwa na  mwelekeo ambao tunaamini  kwamba  kila  taifa kuelekea  katika  njia  yake  kutaleta mafanikio  ya  baadaye.

Mwezi  Septemba 2017 , Ujerumani  itafanya  uchaguzi  mkuu. Merkel  pia alidokeza  hilo  katika  hotuba  yake  ya  mwaka  mpya. Demokrasia  ya bunge  inahitaji "upinzani  na  ukosoaji," lakini  hali  hiyo  inapaswa  kuwa  ya amani  na  kuheshimiana.

"Nina  nia  ya  kushiriki  katika  hatua  za  kisiasa  ambazo  zitashuhudia mijadala ya  amani  miongoni  mwa  raia  wa  kidemokrasia ambao  kamwe hawasahau  heshima  kubwa  iliyopo  kuhudumia  demokrasia  yetu  na  watu wake," alisema.

Mwandishi: Sabine Kinkartz (dr) Sekione Kitojo

Mhariri: Isaac Gamba

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW