1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merz achaguliwa tena kwama mwenyekiti wa chama cha CDU

21 Februari 2026

Chama tawala cha kihafidhina nchini Ujerumani, Christian Democratic Union (CDU), jana kilimchagua tena Kansela Friedrich Merz kuwa mwenyekiti wake.

38. Mkutano wa CDU- Stuttgart 2026 | Friedrich Merz
Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz akihutubia mkutano wa chama cha CDU mjini Stuttgart Ujerumani Februari 20, 2026Picha: Thilo Schmuelgen/REUTERS

Merz aliungwa mkono na asilimia 91.7 za kura za wajumbe 878 kati ya 963 zilizopigwa kwenye mkutano mkuu wa chama hicho huko Stuttgart.

Haya yalikuwa matokeo yake ya pili bora. Mnamo mwaka 2022, alichaguliwa kwa 94.6% ya kura kwenye mkutano wa chama hicho ulioandaliwa kwa njia ya video na baadaye kuthibitishwa kwa asilimia 95.3 ya kura kwa njia ya posta. Mwaka 2024, alipata 89.8% ya kura.

Baada ya kura hiyo, Merz aliwashukuru wajumbe hao na kuahidi ushirikiano bora zaidi ndani ya chama hicho.

Mkutano huo wa siku mbili umefanyika mwanzoni mwa mwaka wa uchaguzi wenye shughuli nyingi kwa CDU, huku chaguzi tano za majimbo zikitarajiwa kufanyika, mwezi Machi na Septemba, hali ambayo huenda ilichangia chama hicho kumuunga mkono Merz.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW