UchumiChina
Merz aenda China kufanya mazungumzo na Rais Xi
24 Februari 2026
Matangazo
Shirikisho la Viwanda vya Ujerumani (BDI) kupitia mjumbe wake Wolfgang Niedermark limemtaka Merz "kushughulikia waziwazi masuala kama vile uwezo kupita kiasi, upotoshaji kwenye ushindani na udhibiti wa mauzo ya nje ya malighafi muhimu.
Ametahadharisha ikiwa hakutakuwa na mabadiliko ya mwelekeo kwa upande wa China, ni wazi kutaibuka migogoro mipya ya kibiashara na Umoja wa Ulaya.
Merz anaondoka Jumatatu kwenda China kwa ziara yake ya kwanza tangu alipokuwa kansela mwaka uliopita na anatarajiwa kujadiliana na Xi masuala kuanza ushirikiano wa kiuchumi hadi ya usalama kama vita vya nchini Ukraine.