1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merz ahofia Ujerumani kumpoteza mshirika wake Marekani

25 Septemba 2025

Kansela Friedrich Merz amesema Ujerumani iko hatarini kumpoteza Marekani kama mshirika wake mkubwa kabisa na wa kumtegemea.

Ujerumani Berlin 2025 | Friedrich Merz akiwa kwenye vikao vya bunge la 27 la Ujerumani
Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz akizungumza kwenye vikao vya bunge la ujerumani, Septemba 24, 2025Picha: Andreas Gora/picture alliance

Kansela Merz amesema hayo jana Jumatano alipokuwa akilihutubia muungano wa tasnia ya kemikali na dawa mjini Berlin.

Amesema changamoto za mazingira ya sasa ya kimaeneo na kisiasa zinazoshuhudiwa sasa hujitokeza kwa nadra sana, na kuongeza kuwa anafanya kila juhudi "kurejesha" uhusiano na Marekani, hasa katika NATO na mahusiano ya kiuchumi.

Rais Donald Trump wa Marekani kwenye hotuba yake mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne, aliwadhihaki washirika wake wa NATO kwa kushindwa kuacha kununua mafuta ya Urusi, akiahidi kuliwekea vikwazo vikali taifa hilo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW