1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merz aonya kuwa Putin anapima subra ya Ulaya

17 Septemba 2025

Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz, ameihimiza Ulaya kutoruhusu Urusi kuamua masharti ya makubaliano ya amani na Ukraine, akionya kwamba kufanya hivyo kutampa Rais Vladimir Putin motisha wa kutafuta shabaha mpya.

Kansela wa Ujerumani, Friedrich Merz akizungumza wakati wa mjadala wa bajeti katika bunge la Ujerumani mnamo Septemba 9, 2025
Kansela wa Ujerumani, Friedrich MerzPicha: Lisi Niesner/REUTERS

Akiwahutubia wabunge leo katika bunge la Ujerumani kama sehemu ya wiki ya bajeti, Merz amesema kwa muda mrefu, Putin amekuwa akipima subira ya Ulaya kwa kuhujumu, kupeleleza, kuuwa na kujaribu kuwatatiza watu.

Kansela huyo ameongeza kusema hii imekuwa dhahiri wiki iliyopita nchini Poland, wakati droni za Urusi zilipoingia kinyume cha sheria kwenye anga ya nchi hiyo na kudunguliwa katika eneo hilo kwa mara ya kwanza.

Merz ameonya kuwa Putin alikuwa akitafuta kuyumbisha jamii ya Wajerumani.

Hata hivyo amesisitiza kuwa hawataruhusu hilo kutokea na kusema Ujerumani inaimarisha uwezo wake wa ulinzi .

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW