Merz awania kuchaguliwa tena kama mwenyekiti wa CDU
20 Februari 2026
Matangazo
Merz anasaka uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa wajumbe wa chama hicho kwa mara ya kwanza tangu kuwa kansela mnamo mwezi Mei mwaka 2025.
Wajumbe pia wataipigia kura hoja kutoka kwa kamati kuu ya utendaji, ambayo CDU inataka kutetea mabadiliko mapya katika soko la nyumba.
Kansela wa zamani, Angela Merkel, pia anatarajiwa kuhudhuria kongamano hilo la siku mbili kama mgeni rasmi, hii ikiwa ni mara yake ya kwanza kushiriki mkutano wa chama cha CDU tangu alipoondoka madarakani mwaka 2021.