1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merz awasili Ukraine kwa mazungumzo

9 Desemba 2024

Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Ujerumani cha CDU, Friedrich Merz, amewasili nchini Ukraine kwa ajili ya mazungumzo na viongozi wa taifa hilo kuhusu namna ya kukabiliana na uvamizi wa Urusi.

Unions Chef Merz in der Ukraine
Picha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Merz amesema baada ya kuwasili mjini Kyiv kuwa anataka kuihakikishia Ukraine kuwa chama chake cha kihafidhina kinaiunga mkono.

Amesisitiza kuwa vita vya Ukraine havina budi kumalizika na amani inapaswa kurejeshwa barani Ulaya.

Kiongozi huyo wa CDU amekuwa akionesha upinzani zaidi dhidi ya Urusi kuliko Kansela Olaf Scholz akisema kuwa Ujerumani inapaswa kuipa Ukraine makombora ya masafa marefu aina ya Taurus.

Ukraine imekuwa ikiyasubiri makombora hayo kwa muda mrefu ili kuyatumia kama Kremlin haitoacha kuishambulia miundombinu yake ya kiraia.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW