MigogoroMashariki ya Kati
Merz: Hakuna mpango unaoeleweka wa kumaliza vita Iran
10 Machi 2026
Matangazo
Akizungumza mjini Berlin akiwa pamoja na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Czech Andrej Babis, Merz amesema kadri siku zinavyosonga mbele inaonesha kuna hatari ya mzozo huo kutanuka na hakuna mpango unaoeleweka wa kuumaliza.
Kiongozi huyo amesema ijapokuwa Ulaya inao mtizamo wa pamoja na Marekani na Israel linapohusika suala la Iran, lakini bara hilo haliko tayari kushuhudia vita visivyo na ukomo.
Pia amesema Ujerumani haitamani kuona Iran inasambaratika na kuzusha taathira mfano wa zile zilizoshuhudiwa baada ya vita vya Libya, Iraq na nchi nyingine kwenye kanda hiyo.