1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merz kukutana na Netanyahu mjini Jerusalem

7 Desemba 2025

Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz anatarajiwa kukutana leo na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu mjini Jerusalem katika ziara yake ya kwanza Israel tangu aingie madarakani mwezi Mei mwaka huu.

Israel Jerusalem 2025 | Friedrich Merz na Benjamin Netanyahu
Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz (kushoto) na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu (kulia) wakutana kabla ya mazungumzo mjini Jerusalem mnamo Desemba 7, 2025Picha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Merz amedokeza kuwa mchakato wa amani huko Gaza utakuwa mojawapo ya masuala ya kipaombele katika ajenda ya mkutano wake na Netanyahu.

Changamoto za mahusiano baina ya nchi hizo mbili pia zitajadiliwa, baada ya Merz kuweka kizuizi kwa baadhi ya silaha zinazouziwa Israel katika kukabiliana na operesheni inayofanywa na jeshi la Israel katika Ukanda wa Gaza .

Merz pia anatazamiwa kuangazia suala linalokithiri la chuki dhidi ya Wayahudi nchini Ujerumani.

Hivi karibuni, balozi wa Israel nchini Ujerumani, Ron Prosor, alionya juu ya chuki ya mrengo wa kushoto kwa Wayahudi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW