1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merz, Macron kushinikiza kuhusu uhuru wa kidigitali wa Ulaya

18 Novemba 2025

Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron watakutana leo kushinikiza kuwepo kwa "uhuru" wa kidijitali wa Ulaya na kupunguza utegemezi wa kampuni kubwa za teknolojia za Marekani.

Ufaransa | Ujerumani mkutano wa baraza la mawaziri mjini Toulon 29.08.2025  | Merz Macron
Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz (kushoto) na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (kulia)Picha: Manon Cruz/REUTERS

Viongozi hao wa mataifa yenye uchumi mkubwa zaidi barani Ulaya watatoa wito huo katika mkutano mjini Berlin, ambao pia utahudhuriwa na wakurugenzi wakuu wa kampuni kubwa za kikanda ikiwa ni pamoja na kampuni ya Ufaransa ya Mistral na kampuni kubwa ya programu ya Ujerumani, SAP.

Ujumbe mkuu wa mkutano mjini Berlin

Hapo jana, Waziri wa Dijitali wa Ujerumani, Karsten Wildberger, alisema ujumbe wa msingi wa mkutano huo utakuwa kwamba "Ulaya iko tayari kuunda mustakabali wake wa kidijitali, ili kupunguza utegemezi".

Badaye wiki hii, Umoja huo wa Ulaya utapendekeza kurejeshwa kwa sheria kuhusu matumizi ya akili mnemba na ulinzi wa data, mada ambayo inatarajiwa kuangaziwa sana katika mkutano wa leo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW