1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merz na Macron kupigania “uhuru wa kidijitali” wa Ulaya

19 Novemba 2025

Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron wameapa kusaidia Ulaya kujiimarisha katika kasi ya Akili Mnemba na kuliondoa bara hilo kwenye utegemezi wa makampuni makuu ya teknolojia ya kigeni

Ujerumani Berlin 2025 | Mkutano wa kilele kuhusu uhuru wa kiteknolojia wa Ulaya na Macron na Merz
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (katikati) na Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz wakitoa maoni yao katika mkutano kuhusu uhuru wa kiteknolojia wa Ulaya, mnamo Novemba 18, 2025 katika Kampasi ya EUREF huko BerlinPicha: Odd Andersen/AFP

Wakizungumza katika mkutano wa kilele mjini Berlin uliowahusisha kampuni za teknolojia za kikanda, viongozi wa uchumi mkubwa zaidi barani Ulaya pia wameahidi kupunguza kanuni zinazodaiwa na kampuni nyingi kuwa zinawazuia kuendelea.Nikimn ukuu hapa Macron anasema: "Ulaya haitaki kuwa mteja wa wajasiriamali wakubwa au suluhu kubwa zinazotolewa ama kutoka Marekani au China, tunataka kwa uwazi kubuni suluhu zetu wenyewe,” akiongeza kuwa msimamo huo unawakilisha "kukataa kuwa vibaraka.” Merzalitoa wito kwa Ulaya kuungana na kujenga njia yake ya kidijitali  na njia hio lazima iendelee kuelekea uhuru wa kidijitali.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW