1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merz: Ningekuwa Kansela ningefanya makubaliano na Trump

10 Novemba 2024

Kiongozi wa chama cha upinzani cha CDU cha Ujerumani Friedrich Merz amesema angekuwa Kansela angejikita katika kutafuta makubaliano na Rais Mteule wa Marekani Donald Trump, yenye maslahi kwa Ujerumani.

Friedrich Merz CDU
Kiongozi wa chama cha upinzani cha Ujerumani cha CDU, Friedrich MerzPicha: IMAGO/Political-Moments

Akizungumza na jarida la Stern la Ujerumani amesema taifa hilo halina budi kutoka kuwa taifa lililolala lenye uwezo wa kati na kuwa taifa linaloongoza lenye uwezo wa kati.

Kiongozi huyo wa CDU aliituhumu serikali ya Ujerumani kwa namna ilivyojihusisha na uchaguzi wa Marekani ambao Trump alishinda. Amedai kuwa Berlin ilipaswa kuwa tayari kwa matokeo hayo lakini badala yake ilichagua kuwa upande wa mgombea wa Democratic, Kamala Harris.

Merz ndiye anayeonekana kuwa na nafasi kubwa zaidi ya kumrithi Kansela Olaf Scholz katika uchaguzi wa mapema unaotarajiwa kufanyika mwakani baada ya serikali ya muungano inayoongozwa na Scholz kuvunjika Jumatano.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW