1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Messi aibeba Barcelona

3 Mei 2021

Lionel Messi hapo Jumapili alifunga magoli mawili na Antoine Griezmann akafunga moja Barcelona walipokuwa wanakwaana na Valencia.

Fußballspieler Lionel Messi 2018
Picha: picture-alliance/empics/N. Potts

Ushindi huo uliwapelekea miamba hao wa Uhispania kupunguza tofauti ya pointi kati yao na vinara Atletico Madrid hadi kufikia pointi mbili.

Atletico Madrid kwa sasa wana pointi 76 kileleni wakifuatwa kwa karibu na Real Madrid walio na pointi 74 sawa sawa na Barca ila barcelona wamedunishwa na uchache wa magoli.

Kwa sasa zimesalia mechi nne katika La Liga na mwishoni mwa wiki hii kutakuwa na mechi muhimu ambayo huenda ikaamua ni nani atakayeibuka na ubingwa wa ligi hiyo wakati Barcelona watakapokuwa nyumbani kuwaalika Atletico Madrid.

Alfred Schreuder ni kocha msaidizi wa Barcelona.

"Hatuhitaji kutazama timu zengine lakini nafikiri uko??? sasa kwa kusema kinyang'anyiro ni kikali na labda tutapoteza pointi, labda Atletico au Real Madrid, Valencia au hata Sevilla ila nafikiri mechi ya wiki ijayo haitokuwa fainali, bado tuna mechi nyengine nne," alisema Schreuder.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW